rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Indonesia Korea Kaskazini Kim Jong Un

Imechapishwa • Imehaririwa

Mauaji ya Kim Jong-nam: Mtuhumiwa aachiwa huru

media
Siti Aisyah alikuwa anashtumiwa sawa na Doan Thi Huong, raia wa Vietnam mwenye umri wa miaka 30, kuwa alimwagia usoni Kim Jong-nam tindikali aina ya VX, ambayo ni sumu kali, Februari 13, 2017 katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia. REUTERS/Lai Seng Sin

Mahakama ya Malaysia imeiachana na kesi dhidi ya raia wa Indonesia anayeshtumiwa kuhusika katika mauaji ya Kim Jong-nam, kaka wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, aliyeuwana mnamo mwaka 2017.


Siti Aisyah, mwenye umri wa miaka 26, ameachiwa huru na ataweza kurudi nyumbani, amesema mwendesha mashitaka mkuu.

Siti Aisyah alikuwa anashtumiwa sawa na Doan Thi Huong, raia wa Vietnam mwenye umri wa miaka 30, kuwa alimwagia usoni Kim Jong-nam tindikali aina ya VX, ambayo ni sumu kali, Februari 13, 2017 katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia.

Leo Jumatatu waendesha mashitaka wametoa taarifa mbele ya mahakama kuwa wamepewa maagizo ya kuachana na mashitaka ya mauaji dhidi ya Siti Aisyah, bila kutoa maelezo zaidi.

Katika barua ya tarehe 8 Machi mwaka huu, iliyotumwa kwa Waziri wa Sheria, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Malaysia Tommy Thomas, alibaini kwamba amefanya hivyo kufuatia ombi viongozi wa serikali nchini Indonesia.

Ingawa mashtaka ya mauaji yamefutwa, mahakama imefutilia mbali ombi la wanasheria wake wa kufutiwa mashitaka yote yanayomkabili."Sisi bado

Tunaamini kwamba mteja wetu alitaka kutolewa tu kama kafara," mmoja wa wakili wa Siti Aisyah, Gooi Mara Seng, ameviambia vyombo vya habari, huku akiongeza "bado nadhani Korea Kaskazini inahusika na hilo."