rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

India Majanga ya Asili

Imechapishwa • Imehaririwa

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko yafikia 370 Kerala, India

media
Mvulana huyu amuokoa mtoto mchanga kwa kuepuka mafuriko kaskazini mashariki mwa India. REUTERS/Stringe

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko makubwa katika vijiji kadhaa katika jimbo la Kerala, Kusini Magharibi wa nchi ya India, imefikia 370. Kuna uhaba wa maji safi ya kunywa na watu wengi wanateseka kutokana na magonjwa yanayosababishwa na mafuriko, kwa mujibu wa mashirika yanayotoa misaada,.


Watu wengine 700,000 wameyakimbia makwao baada ya makaazi yao kusombwa na maji.

Maafisa wa ukoaji wanasema bado wanawatafuta maelfu ya watu ambao hawajapatikana hadi sasa, huku kukiwa na wasiwasi kuwa, huenda idadi ya watu waliopoteza maisha ikaongezeka.

Vikosi vya uokoaji nchini humo wanasema wanatarajia kuopoa miili ya watu wengi zaidi.

Maji yamezingira kila kona ya mji kutokana na mvua kali huku nyumba za makaazi zile za biashara pamoja na barabara zimeharibiwa vibaya.