rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Thailand

Imechapishwa • Imehaririwa

Wengi wa wavulana 12 waliokwama pangoni waokolewa Thailand

media
Magari ya wagonjwa yakiondoka eneo kunakoendeshwa shughuli ya uokoaji wa watoto 12 waliokwama pangoni Thailand. REUTERS/Soe Zeya Tun

Zoezi la uokoaji wa wavulana 12 na kocha wao wa soka waliokwama pangoni huko Mae Sai, nchini Thailand, kwa siku 15, lilianza Jumapili hii, Julai 8 na linatarajiwa kuendelea Jumatatu wiki hii.


Wavulana nane wameokolewa wakiwa hai ndani ya pango lililojaa maji kabla ya jitihada za uokoaji kusitishwa kwa muda katika kazi hiyo inayotajwa kuwa ni hatari kwa waokoaji pia kwani tayari mzamiaji mmoja amefariki dunia katika kazi hiyo.

Afisa wa Wizara ya Ulinzi alikuwa ameeleza kuwa watoto sita waliokolewa. Zoezi la uokoaji liliendeshwa kwa kasi zaidi kuliko ilivyotarajiwa, kwa upande wa serikali, ni muhimu kuchukua hatua haraka. Zoezi hili linaendeshwa haraka ikiwa imesalia siku chache tu kabla ya mvua kuanza tena kunyesha.

Wazamiaji kutoka nchi mbalimbali wamewasili Thailand,kusaidia kazi hiyo,huku wazazi wa watoto hao wakiwa katika hali ngumu na kuomba kila linalowezekana lifanyike kunusuru maisha ya watoto wao.

Watoto hao na kocha wao waliingia ndani ya pango hilo kufanya utalii.

Mamilioni ya lita za maji yamekwisha kutolewa kutoka ndani ya pango hilo,ili kurahisisha kazi ya uokoaji.

Shughuli za uokoaji wa watoto waliokwama pangoni zinatarajia kuendelea Jumatatu wiki hii.