Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-KASKAZINI-MAREKANI

Korea kaskazini yaahidi kusimamisha majaribio ya silaha zake za nyuklia

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amepongeza ahadi ya Korea kaskazini kusimamisha majaribio yake ya kinyuklia na ufyatuaji wa makombora huku akitoa angalizo kuwa Tokyo itaendelea kuishinikiza zaidi serikali ya Pyongyang.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un KCNA/via REUTERS/File Picture
Matangazo ya kibiashara

Abe amesema hatua hiyo inatia matumaini lakini cha muhimu ni utekelezwaji kufanyika kwa ukweli na kwa namna inayokubalika.

Hayo yanajiri baada ya Kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un jumamosi hii kuahidi kwamba taifa lake litasimamisha majaribio yake ya kinyuklia hatua iliyopongezwa na Marekani na Korea Kusini.

Tamko hilo la Korea Kaskazini linakuwa hatua muhimu katika kutatua mzozo wa kidiplomasia kati ya Korea Kaskazini na mataifa ya magharibi.

Hatua hii inakuja katika kipindi kisichozidi juma moja kabla ya kiongozi wa Korea Kaskazini kukutana na wa kusini Moon Jae-in kwa ajili ya mazungumzo ya kuharibu silaha za nyuklia kuelekea mkutano unaosubiriwa kwa hamu kati yake na raisi wa Marekani Donald Trump.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.