Pata taarifa kuu
SUDANI-USALAMA

Sudani: Wanamgambo wa Boko Haram wakamatwa Darfur

Jeshi la Sudan limedai kuwa limewakama watu sita Magharibi mwa nchi, karibu na mpaka wa Chad. Watu hao wanatuhumiwa kuwa ni wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram, kutoka kaskazini mwa Nigeria.

Jeshi la Sudan huko Darfur, Novemba 2019.
Jeshi la Sudan huko Darfur, Novemba 2019. © ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Khartoum inasema watu hao sita wamekuwa wanatumia pasi kusafiria za Chad. "Kwa kuwa tuna makubaliano ya usalama, wamekabidhiwa kwa serikali ya Ndjamena," jeshi la Sudani limesema.

Boko Haram kuwa na watu kutoka Chad katika wapiganaji wake sio jambo la kushangaza. Kulingana na shirika la kimataifa linalohusika na kutatua migogoro (ICG), wengi mwa raia hawa wanachunguzwa kwa muda mrefu na wengine wamefungwa jela mapema mwaka 2011. Walakini, kuwakamatia nchini Sudan ni jambo la kushangaza, kwani eneo hilo ni mbali na ngome yao.

Kwa mujibu wa mtafiti, Khartoum ingefikiria kuhusu kuunda kikosi kitakachozuia kuingia nchini Sudan kwa wanamgambo wa kundi hilo la Waisilamu. Itakumbukwa kwamba mwezi Septemba, Sudan iliagiza kufungwa kwa mpaka wake na Jamhuri ya Afrika ya Kati na Libya, ikibaini kwamba kuna hatari za kiuchumi na usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.