Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-WAASI-UCHAGUZI

Umoja wa Mataifa wasema zaidi ya watu 300,000 wamekimbia makwao Mashariki mwa DRC

Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu 300,000 wamekimbia makwao Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu kuanzia mwezi Juni kwa sababu ya mapigano ya kikabila.

Wanajeshi wa DRC wakishika doria Mashariki mwa DRC
Wanajeshi wa DRC wakishika doria Mashariki mwa DRC Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hali hii inazua wasiwasi kwa watalaam wa afya kufanikisha mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola, ambao umesababisha zaidi watu zaidi 1,000 kupoteza maisha katika jimbo la Kivu Kaskazini tangu mwezi Agosti mwaka 2018.

Machafuko ya kikabila yameendelea kushuhudiwa kati ya kabila la Lendu na Hema katika mkoa wa Ituri, na kusababisha watu 161 kupoteza maisha kwa kipindi cha wiki moja.

" Machafuko Kaskazini Mashariki mwa DRC yamesababisha watu 300,000 kuyakimbia makwao tangu mapema mwezi Juni. Hali imeendelea kuwa mbaya katika mkoa wa Ituri, kutokana na mapigano kati ya makabila ya Hema na Lundu,” amesema msemaji wa Tume inayoshughulikia wakimbizi,  Babar Baloch.

Mzozo katika jimbo la Kivu ulianza mwaka 2004 baada ya jesji la serikali FARDC kuanza kukabilana na waasi wa Kihutu wanaofahamika kama FDLR.

Mbali na FDLR, makundi mengine ya waasi ambayo yameendela kusababisha ukosefu wa usalama ni pamoja na ADF Nalu, Mai Mai.

Kundi la M 23 tayari limeshindwa katika harakati zake sawa na CNDP.

Ukosefu wa usalama Mashariki mwa DRC, umesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine zaidi ya Millioni 1 kuyakimbia makwao kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.