Pata taarifa kuu
GABON-SIASA-USALAMA

Askari waliojaribu kufanya mapinduzi ya kijeshi wakamatwa Gabon

Vyombo vya usalama nchini Gabon vimefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi la hapo jana ambapo kiongozi wa wanajeshi walioshiriki jaribio hilo amekamatwa na wengine wawili wameuawa.

Vikosi vya usalama vya Gabon vikipiga doria katika maeneo jirani na makao makuu ya Radio na Televisheni ya taifa, ambapo kundi la wanajeshi walivamia wakijaribu kuipindua serikali, Januari 7, 2018.
Vikosi vya usalama vya Gabon vikipiga doria katika maeneo jirani na makao makuu ya Radio na Televisheni ya taifa, ambapo kundi la wanajeshi walivamia wakijaribu kuipindua serikali, Januari 7, 2018. © Steve JORDAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jaribio hili limekashifiwa vikali na viongozi wa umoja wa Afrika, umoja wa Ulaya na umoja wa Mataifa ambao wamesema hakuna demokrasia itakayopatikana kwa nguvu ya kijeshi au kupitia mapinduzi.

Hali ya utulivu imerejea nchini humo huku usalama ukiwa umeimarishwa kwenye maeneo mengi ya nchi kwa mujibu wa msemaji wa Serikali ya Gabon, Guy Betrand Mapangou.

Balozi wa Gabon nchini Ufaransa, Flavien Enongoue, amesema uchunguzi tayari umeanza kubaini wanajeshi zaidi waliohusika.

Kwa upande wa msemaji wa kinara wa upinzani nchini humo Jean Ping, Laurence Ndong, amesema wao wameelewa kwanini wanajeshi hao walijaribu kuipindua Serikali.

Jaribio hili limefanyika wakati huu Rais Ali Bongo akiwa nchini Moroco ambako anapatiwa matibabu kwa zaidi ya miezi miwili sasa tangu aanze kuugua akiwa nchini Saudi Arabia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.