Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Watu zaidi ya 12 wauawa katika shambulio nchini Mali

Watu zaidi ya 12 kutoka jamii ya Tuareg wameuawa na kundi la watu wasiojulikana kaskazini mashariki mwa Mali karibu na mpaka na Nigeria. Mashahidi wanasema washambuliaji walikuwa kwenye pikipiki

Askari wa Mali mbele ya helikopta iliyombeba Waziri Mkuu wa Mali, Menaka, Mei 9, 2018.
Askari wa Mali mbele ya helikopta iliyombeba Waziri Mkuu wa Mali, Menaka, Mei 9, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Takribani watu 200, wengi wao wakiwa ni raia wa kawaida, hasa kutoka jamii za Fulani na Tuareg, wameuawa tangu mwanzoni mwa mwaka huu katika eneo hilo, ambako mapigano yanaendelea kati ya kundi la wanajihadi wenye mafungamano na kundi la Islamic State (IS) na makundi mawili ya wapiganaji hasa kutoka jamii ya Tuareg (Gatia na MSA) yanayosaidiwa na kikosi cha askari wa Ufaransa (Barkhane) pamoja na jeshi la Mali.

Shambulizi lilitokea kilomita 45 magharibi mwa Menaka, jiji kuu la ukanda huo, kwa mujibu wa afisa aliyechaguliwa katika eneo hilo, chanzo cha usalama wa ndani na taarifa kutoka kwa kundi la wapiganaji la MSA (Movement for the Salvation of Azawad, kutoka kundi la zamani waasi).

"Watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki waliua leo (Jumanne) raia kumi na wawili," afisa huyo aliliambia shirika la Habari la AFPakinukuu mkaazi mmoja wa mji huo alioshuhudia tukio hilo. "Kwa sasa, hatujui waliohusika na amauaji hayo, sijui kama ni matokeo ya migogoro kati ya makabila, au kitendo cha kigaidi."

Chanzo cha usalama wa eneo hilo kimethibitisha "mauaji ya raia wasiopungua 12", kikiongeza kuwa "baadhi ya vyanzo vinasema kumi na mbili, vingine kumi na sita". "Vijana ni miongoni mwa watu wengi waliouawa".

Katika taarifa yake, kundi la wapiganaji la MSA limesema kuwa "watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki waliua raia 17 kutokaa kambi mbili za watu kutoka jamii ya Tuareg.

Katika ripoti ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Agosti, kundi la wataalam lilibainisha kuwa migogoro kati ya jamii katika kanda hiyo, kuhusu nyadhifa serikalini, udhibiti wa maeneo ya kibiashara, malisho na kumiliki visima, kumeongeza mvutano unaotokana na mapigano kati ya wanajihadi na majeshi ya kimataifa na yale ya Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.