Pata taarifa kuu
ANGOLA-HAKI

Mtoto wa rais wa zamani wa Angola dos Santos afungwa kwa madai ya rushwa

Mtoto wa rais wa zamani wa Angola Jose Eduardo Dos Santos, Jose Filomeno Dos Santos, amezuiwa kwa muda kutokana na kesi ya rushwa ya Dola milioni 500 ambapo hakimu mkuu wa jamuhuri amesema kuzuiliwa kwake ni kutokana na ugumu wa kesi.

Mjini kati Luanda, mji mkuu wa Angola (picha ya kumbukumbu).
Mjini kati Luanda, mji mkuu wa Angola (picha ya kumbukumbu). Getty Images/Kostadin Luchansky - Angola Image Bank
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwanasheria mkuu nchini Angola, uchunguzi umeanza na kwamba kuzuiliwa kwa Jose Filomeno Dos Santos ni kutokana na ugumu wa kesi lakini pia ni kutaka kuweka wazi kesi hii kuhakikisha pia ufanisi katika uchunguzi.

Mwanasheria huyo amesema kuna ushahidi tosha unaothibitisha kuwa watuhumiwa walijihusisha katika rushwa.

Kujitajirisha kinyume cha sheria na utapeli ni miongoni mwa makosa yaliotajwa na ambayo kifungo chake ni miaka 8 au 12 jela.

Jean Claude Bastros de Morais, mtu wa karibu na mtoto wa Dos Santos naye pia ametiwa kizuizini. Mfanyabiashara huyo mwenye uraia pacha wa Angola na Usuisi anatajwa kuwa aliongoza sehemu ya fuko la fedha za taifa dola bilioni 5 ambazo Jose Filomeno dos Santos alikuwa akiongoza kuanzia mwaka 2013 hadi 2018 ambapo anatuhumiwa kuongoza vibaya fuko hilo.

Msemaji wa chama cha upinzani nchini Angola UNITA Alicides Sakala amepongeza hatua hiyo na kueleza kwamba chama cha UNITA kimekuwa kikipiga kelele kuhusu swala la rushwa na kwamba ni miongoni mwa ahadi za rais wa nchi hiyo wakati wa kampeni za uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.