Pata taarifa kuu
MISRI-SUDANI-SIASA-USALAMA

Kiongozi wa upinzani Sudani azuiwa kungia Misri

Kiongozi wa upinzani nchini Sudani Sadiq al-Mahdi, amezuiwa katika uwanja wa ndege wa Cairo kuingia nchini Misri. Serikali ya Misri haijazungumza chochote kuhusina na tukio hilo.

Kiongozi wa Omar al-Bashiri, Sadiq al-Mahdi, amezuiliwa kuingia nchini Misri.
Kiongozi wa Omar al-Bashiri, Sadiq al-Mahdi, amezuiliwa kuingia nchini Misri. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Chama cha UMMA kimethibitisha kuzuiwa kwa kiongozi wake, ambaye amekuwa akiishi nchini Misri kwa miaka miwili kwa sababu za kisiasa.

Mahdi alirejea Sudani mwaka uliopita, lakini ameendelea kuishi Misri na alikuwa ameondoka kwenda jijini Berlin nchini Ujerumani kuhudhuria kongamano la wanasiasa wa upinzani.

Mwanasiasa huyo mkongwe ambaye amewahi pia kuwa Waziri Mkuu wa Sudani amelazimika kwenda nchini Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.