Pata taarifa kuu
SIERRA LEON-UCHAGUZI-MATOKEO

Mgombea wa upinzani nchini Sierra Leone aongoza huku duru ya pili ikitarajiwa

Matokeo ya awali yanayoendelea kutangazwa nchini Sierra Leone, yanaonesha kuwa mgombea wa upinzani anaongoza dhdi ya mgombea wa chama tawala kwa zaidi ya kura elfu 15.

Mgombea wa urais kupitia chama cha upinzani Julius Maada Bio, alivyopiga kura tarehe 7 mwezi Machi 2018
Mgombea wa urais kupitia chama cha upinzani Julius Maada Bio, alivyopiga kura tarehe 7 mwezi Machi 2018 REUTERS/Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Mgombea wa upinzani Julius Maada Bio amepata asilimia 43.5 ya kura dhidi ya asilimia 42.6 alizopata mgombea wa chama tawala Samura Kamara huku tume ya uchaguzi ikiwa imehesabu karibu asilimia 75 ya kura zote.

Muungano wa kitaifa unaoongozwa na mwanadiplomasia wa zamani kwenye umoja wa Mataifa Kandeh Yumkella ambaye anatarajia kugawa kura za wagombea vinara, yeye amepata asilimia 6.69 ya kura zote.

Matokeo rasmi ya uchaguzi uliofanyika juma lililopita yanatarajiwa kutangazwa ndani ya siku chache zijazo lakini kwa matokeo haya ni wazi kuwa huenda kukawa na duru ya pili ya uchaguzi kwa kuwa hakuna mgombea ambaye huenda akafikisha ushindi wa asilimia 55 unaotakiwa kikatiba.

Iwapo kutakuwa na duru ya pili itafanyika baada ya wiki mbili, baada ya matokeo ya mwisho kutangazwa.

Tume ya Uchaguzi imeendelea kutoa wito wa uvumilivu kwa wananchi wa taifa hilo wakati huu ikiendelea kujumuisha matokeo.

Waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi wakiwemo wale wa umoja wa Ulaya wamesema uchaguzi wa juma lililopita ulikuwa huru, wakuaminika na ulioandaliwa vizuri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.