Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-SIASA-UCHUMI

Bunge la Afrika Kusini kujadili utaratibu wa kumuondoa madarakni Zuma

Bunge nchini Afrika Kusini juma hili linatarajiwa kuketi kujadili hatua za kuchukua kumuondoa rais Madarakani wakati huu shinikizo zaidi likiongezeka kwa rais Jacob Zuma kujiuzulu.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aendelea kukabiliwa na kashfa mbalimabali, na hivyo kupoteza imani kwa baadhi ya wabunge kutoka chama tawala cha ANC.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aendelea kukabiliwa na kashfa mbalimabali, na hivyo kupoteza imani kwa baadhi ya wabunge kutoka chama tawala cha ANC. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa bunge umekuja ikiwa ni siku chache tu zimepita toka mahakama ya katiba nchini humo kuamua kuwa bunge lilishindwa kumuwajibisha rais Zuma kwa matumizi mabaya ya fedha za uma kufanya ukarabati kwenye makazi yake binafsi.

Mwezi uliopita mahakama ilimkuta na hatia ya kukiuka hati ya kiapo kwa kukataa kurejesha kiasi cha fedha alichotakiwa kurudisha na kuliagiza bunge kuandaa mchakato utakaotumika kumuondoa madarakani.

Rais Zuma anaendelea kukabilia na kashfa ya ufisadi, huku chama cha Nelson Mandela kikiendelea kupoteza wafuasi katika majimbo mbalimbali nchini humo.

Julius Malema mkosoaji na mpinzani mkubwa wa Jacob Zuma amekua akihamasisha wabunge wenzake kuchukua uamuzi wa kumng'atua madarakani Bw Zuma, bila mafanikio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.