Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Ni Dlamin-Zuma au Ramaphosa kuwa kiongozi mpya wa chama cha ANC

Chama tawala nchini Afrika Kusini, ANC Jumatatu hii kinatarajiwa kupiga kura kuchagua kiongoz mpya wa chama atakayechukua nafasi ya rais Jacob Zuma.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ANC, 17 Desemba 2017
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ANC, 17 Desemba 2017 REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mvutano wa muda mrefu kuhusu namna zoezi la upigaji kura litakavyofanyika, hatimaye wanachama wa chama tawala nchini Afrika Kusini ANC wamekubaliana na kupitisha majina mawili ya watu watakaowania kuwa kiongozi wa chama.

Wajumbe wa mkutano mkuu wamepitisha majina ya makamu wa rais Cyril Ramaphosa pamoja na aliyekuwa mkuu wa tume ya umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma, ambao sasa wanatarajiwa kupigiwa kura hivi leo kupata mshindi.

Wagombea wote wawili wanapewa nafasi ya kila mmoja kuibuka mshindi kutokana na Sera zao ambapo wote wameahidi kuleta umoja ndani ya chama na kupambana na masuala ya ufisadi.

Nkosazana Dlamini-Zuma anajivunia rekodi yake ya utendaji kazi katika umoja wa Afrika pamoja na sera yake ya kutaka kurejesha mashamba kwa watu weusi, sera ambayo inaonekana kumpa umaarufu.

Hata hivyo wachambuzi wengi wa siasa za Afrika Kusini wanasema dosari kuu aliyonayo Nkosazana ni kutokana na ukweli kuwa yuko karibu sana na rais Jacob Zuma ambaye aliwahi kuwa mke wake nyakati fulani.

Kwa upande wa makamu wa rais Cyril Ramaphosa yeye anaungwa sana mkono na watu wa kipato cha kati ambao wengi wanaona kuwa atafaa sana katia chama kutokana na msimamo wake wa kupiga vita masuala ya rushwa ndani ya chama.

Kinachosubiriwa sasa ni uamuzi wa wajumbe wa chama cha ANC kuamua nani atakuwa kiongozi wao wa chama kati ya wagombea hawa wawili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.