rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uhispania EU

Imechapishwa • Imehaririwa

Kampuni ya Uber yapata pigo jingine, mahakama ya Ulaya yasema ni kampuni ya Tax

media
Nembo ya kampuni ya Uber inayotoa huduma za usafiri kupitia mtandao REUTERS

Mahakama ya juu kwenye umoja wa Ulaya imetoa uamuzi kuwa kampuni ya Uber ni kama kampuni nyingine za usafirishaji na sio programu ya kwenye simu na kwamba Serikali ziiichukulie kama kampuni ya huduma za Tax, uamuzi ambao unaelezwa kuwa pigo kwa kampuni hiyo.


Uamuzi huu wa mahakama ya Ulaya ni pigo kwa kampuni ya Uber yenye makao yake nchini Marekani, kampuni ambayo ilizusha sintofahamu kati yake na madereva wa Tax na maofisa wengine kuhusu kuheshimu sheria za ndani za nchi husika.

Uamuzi huu umekuja katika wiki ambayo moja ya madereva wake walikiri kujaribu kumbaka na kumuua mfanyakazi wa ubalozi wa Uingereza akitokea kwenye ukumbi wa Starehe, mjini Beirut, Lebanon.

“Huduma inayotolewa na Uber kwa kuwaunganisha watu na madereva ambao hawakupewa mafunzo imo ndani ya huduma za usafiri,” imesema hukumu ya mahakama ya Ulaya.

Mahakama hiyo imeongeza kuwa “nchi wanachama sasa zinaweza kuitoza Uber kwa kufuata sheria za utoaji wa huduma za usafiri”.

Kampuni ya Uber ni moja ya makampuni yenye majina duniani ambayo huduma zake zinatolewa kwa njia ya programu maalumu ya kwenye simu, ikisisitiza kuwa inawaunganisha wateja na madereva katika miji zaidi ya 600 duniani.

Kampuni hii imejikuta ikipingwa vikali na makampuni ya Tax kwenye nchi za Ulaya pamoja na washindani wake wengine ambao wanasema huduma yake inakwepa baadhi ya sheria kama vile kupitia mafunzo na utolewaji wa leseni kwa madereva na magari.

Kesi hii ilifunguliwa na umoja wa madereva tax kwenye mji wa Barcelona nchini Hispania, ambapo walidai kuwa Uber ni kama kampuni nyingine ta Tax na wanapaswa kutoa huduma kwa misingi ya sheria za usafiri.

Licha ya kampuni hiyo kudai kuwa uamuzi huu hautaarhiri shughuli zake, bado nchi kadhaa za Ulaya zimeruhusu kutumiwa kwa huduma hii.

Hata hivyi wadadisi wa mambo wanasema uamuzi wa mahakama ya Ulaya utakuwa na madhara katika utendaji na ajira ambazo zilikuwa zimetengenezwa na kampuni hii.

Kampuno ya Uber ilikuwa haijari madereva na badala yake watu binafsi walikuwa na uwezo wa kutumia magari yao binafsi kwa kulipa kamisheni waliyokubaliana na Uber.