Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Kesi ya uhaini dhidi ya kigogo wa upinzani nchini Zambia yahairishwa

Kesi ya uhaini dhidi ya kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema, iliyokuwa imepangwa kuanza leo imeahirishwa hadi siku ya Jumatano.

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia  Hakainde Hichilema
Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema REUTERS/Rogan Ward
Matangazo ya kibiashara

Chama chake cha UPND kinachotaka mashataka dhidi ya kiongozi wao yatupiliwe mbali, kimesema kuwa kesi hiyo imeahirishwa kwa sababu Hakimu ameugua.

Wakati uo huo, mke wa Hichilema, ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kuingia kati kesi hii na kumsaidia mume wake.

Mutinta Hichilema amesema mume wake ameshtakiwa kwa sababu za kisiasa, na kuongeza kuwa hali ya demokrasia nchini humo imeshuka sana.

Soma pia ripoti hii. Bonyeza hapa

Mwezi Aprili, Hichilema alikamatwa kwa madai ya kuzuia msafara wa rais Edgar Lungu.

Hata hivyo, kigogo huyo wa upinzani amekuwa akikanusha madai hayo na kudai kuwa kesi hiyo imechochewa kisiasa.

Rais Lungu naye amekuwa akisema hajawahi kuingilia shughuli za Mahakama hasa dhidi ya mpinzani wake.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.