Pata taarifa kuu
DRC-UNSC

Mende akosoa kauli ya Hollande, UNSC yainyooshea kidole Serikali ya DRC

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, imelaani vikali kauli ya ukosoaji iliyotolewa na mwanzoni mwa juma hili na Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, aliyeituhumu Serikali kuhusika na mauaji ya waandamanaji wa upinzani Jumatatu na Jumanne ya wiki hii.

Waziri wa habari na msemaji wa Serikali ya DRC, Lambert Mende akizungumza hivi karibuni, Alhamisi ya wiki hii amekosoa kauli ya Ufaransa
Waziri wa habari na msemaji wa Serikali ya DRC, Lambert Mende akizungumza hivi karibuni, Alhamisi ya wiki hii amekosoa kauli ya Ufaransa Reuters
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Kinshasa, waziri wa habari na msemaji wa Serikali ya DRC, Lambert Mende, amesema kuwa nchi yake sio kisiwa ama koloni la Ufaransa, na hivyo kiongozi huyo hapaswi kuingilia masuala yake ya ndani.

Waziri Mende amesema kuwa kauli ya Rais Hollande haikuwa inalenga kuhubiri amani kwenye taifa lake bali alilenga kuendelea kuleta mgawanyiko na kuzidisha chuki kati ya upinzani na Serikali.

Serikali inasema kuwa, matamshi ya rais wa Ufaransa yaliegemea taarifa za upande mmoja kwakuwa hata waliompa taarifa huenda hawakushuhidia kile kilichotokea wakati wa maandamano ya upinzani waliokuwa wakishinikiza kuondoka madarakani kwa rais Josephu Kabila.

Kwenye hotuba yake aliyoitoa kwenye baraza la umoja wa Mataifa, Rais Francois Hollande alikashifu nguvu kubwa iliyotumiwa na vikosi vya Serikali kukabiliana na waandamanaji, huku akitaka Serikali ya rais Kabila iandae na kufanya uchaguzi wa amani kwa kufuata misingi ya katiba.

Baadhi ya vijana wakiwa wamechoma matairi kwenye moja ya barabara za Kinshasa
Baadhi ya vijana wakiwa wamechoma matairi kwenye moja ya barabara za Kinshasa https://cdn-images

Katika hatua nyingine, mkuu wa tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, ameelekez lawama za moja kwa moja kwa Serikali ya DRC kwa kuendelea kuchochea mvutano wa kisiasa nchini humo, hali iliyosababisha kushuhudiwa kwa makabiliano makali mwanzoni mwa juma hili jijini Kinshasa.

Zeid Ra’aad Al Hussein amesema kuwa “mamlaka lazima zirudi nyuma dhidi ya kutumia nguvu kwa wapinzani na kutengeneza daraja kati yake,” alisema mkuu huyo.

Kauli yake imekuja ikiwa ni siku chache tu zimepita toka kushuhudiwa kwa vurugu kubwa jijini Kinshasa katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja, ambapo polisi walikabiliana na waandamanaji wa upinzani waliokuwa wakishinikiza rais Kabila aondoke madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.