rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Burundi Pierre Nkurunziza Umoja wa Mataifa UN Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki

Imechapishwa • Imehaririwa

Burundi: chama tawala chamkataa Bathily, mpatanishi wa UN

media
Abdoulaye Bathily, mpatanishi wa Umoja wa Mataifa, mjini Bujumbura Juni 23 mwaka 2015. AFP PHOTO / MARCO LONGARI

Nchini Burundi, chama tawala cha CNDD-FDD, ambacho kimedhamiria kufanya uchaguzi licha ya kupingwa kimataifa, kimeonyesha Jumapili Julai 5 ghadhabu yake dhidi ya jumuiya ya kimataifa, lakini pia dhidi ya mpatanishi wa Umoja wa Mataifa, Abdoulaye Bathily.


Raia huyu kutoka Senegal aliteuliwa kutatua mgogoro nchini Burundi. lakini sasa chama cha CNDD-FDD kumeomba mpatanishi huyu wa Umoja wa Mataifa ajiuzulu.

" Chama cha CNDD-FDD kinafahamisha kwamba kimeondoa imani yake kwa mwakilishi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na kumtaka kuwasilisha barua ya kujiuzulu, kwani alipoteza imani mwenyewe tangu alipoanza kazi yake ", amesema msemaji wamsemaji wa chama tawala cha CNDD-FDD Gelase-Daniel Ndabirabe.

Chama tawala kinamtuhumu Bathily hasa kwa kutokuwa kutoanzisha mikutano yake kwanza na viongozi wa nchi au kupendekeza kuahirishwa kwa uchaguzi. Kwa kifupi "kushindwa kuheshimu uhuru wa taifa. "

Lakini huu kweli si mshangao. Chama cha CNDD-FDD hakikushiriki katika mazungumzo yalioanzishwa na timu ya kimataifa ambapo Abdoulaye Bathily ni miongoni mwa wanaounda timu hiyo ya kimataifa. Serikali ya Burundi, ilishiriki mara moja pekee, huku ikitoa ujumbe uliyo wazi: kamwe hatotokubali kuahirisha kwa mara nyingine tena uchaguzi. Hata hivyo pendekezo hili lilitolewa na timu ya kimataifa, ikiomba uchaguzi wa wabunge na madiwani na ule wa urais uahirishwe hadi Julai 30 ili kuruhusu uchaguzi wa kuaminika. Hoja hii ilitolewa na wasuluhishi ili kupasisha pendekezo hili. Na hoja hiyo ilielezwa na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Abdoulaye Bathily wakati mazungumzo yalishindwa zaidi ya wiki kabla ya kuteuliwa kuwa msuluhishi mpya katika mgogoro unaoendelea nchini Burundi.

Abdoulaye Bathily alieteuliwa kama msemaji wa timu ya usuluhishi. Alisema kuwa katika hali ya sasa, uchaguzi hautakua huru wala wa kidemokrasia. Waziri wa mambo ya Ndani Edouard Nduwimana alimjibu kwa kasi kwenye Idhaa za RFI. Edouard Nduwimana alimtuhumu Abdoulaye Bathily kuwa anaegemea upande fulani na kusema kuwa amejikataa mwenyewe, baada ya kuonesha msimamo wake.

Ripoti ya timu ya wasuluhishi wa kimataifa itakua kwenye meza ya marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambao wanakutana leo Jumatatu Julai 6 jijini Dar es Salaam. Na ripoti hii haikutiliwa saini pekee na Abdoulaye Bathily. Wawakilishi wa Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya nchi za Maziwa Makuu ni wajumbe wa timu hii ya usuluhishi, amabo pia walitia saini kwenye ripoti hii.