Pata taarifa kuu

Ufaransa: Papa Francis aanza ziara yake Marseille, suala la uhamiaji kwenye ajenda ya ziara yake

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis, 86, amewasili siku ya Ijumaa, Septemba 22 huko Marseille, kusini-mashariki mwa Ufaransa, kwa ziara ya siku mbili inayohusu hasa mada ya uhamiaji na Mediterania.

Waziri Mkuu wa Ufaransa Élisabeth Borne na Papa Francis katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Marseille, huko Marignane, Ijumaa hii, Septemba 22, 2023.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Élisabeth Borne na Papa Francis katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Marseille, huko Marignane, Ijumaa hii, Septemba 22, 2023. AFP - ANDREAS SOLARO
Matangazo ya kibiashara

Ndege ya Papa imetua muda mfupi baada ya saa kumi jioni kwa saa za Ufaransa katika uwanja wa ndege wa Marseille-Provence huko Marignane. Akiwa kwenye kiti cha magurudumu, François amepokelewa na Waziri Mkuu wa Ufaransa Élisabeth Borne.

Wakati wa safari yake, kutoka Roma kwenda jiji la Phocaea, kulingana na mwandishi wetu huko Vatican, Camille Dalmas, alisema "Natarajia mengi kutoka kwa safari hii".

Akijibu maswali machache kutoka kwa waandishi wa habari waliokuwa kwenye ndege pamoja naye, alitoa maoni juu ya kuwasili kwa idadi kubwa ya wahamiaji huko Lampedusa ambao waliwasili katika siku za hivi karibuni. Mji alioutembelea mnamo mwaka 2013.

Francis analaani Mediterania kuwa "makaburi" ya wahamiaji. Kwa suala hili alizungumza juu ya ukatili na ukosefu wa ubinadamu.

Akionekana kuguswa, amesikitishwa pia kwamba baada ya kuvuka jangwa, na kukabiliana na wafanyabiashara nchini Libya, wahamiaji hao walitupwa baharini. Maneno ambayo anakusudia kuyapeleka Marseille.

Papa Francis akiwa na wahamiaji na viongozi wa kidini mbele ya ukumbusho maksusi kwa wanaume na wanawake waliotoweka baharini, kwenye Kanisa Kuu la Notre-Dame de la Garde huko Marseille, Ijumaa hii, Septemba 22, 2023.
Papa Francis akiwa na wahamiaji na viongozi wa kidini mbele ya ukumbusho maksusi kwa wanaume na wanawake waliotoweka baharini, kwenye Kanisa Kuu la Notre-Dame de la Garde huko Marseille, Ijumaa hii, Septemba 22, 2023. AFP - ALESSANDRO DI MEO

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani anaelezea jiji hilo kama mlango, dirisha la Mediterania. "Natumai nitakuwa na ujasiri wa kusema kila kitu ninachotaka kusema," alisema dakika ishirini kabla ya ndege yake kutua.

Kumbuka kwamba kiongozi wa Kanisa Katoliki kwa kuwa makini na sababu ya mazingira, Bi. Borne alichukua fursa ya mazungumzo yao mafupi kumpa hati kuhusu mipango ya kiikolojia ya serikali yake.

Papa Francis akiwa Kanisa kuu la Notre-Dame de la Garde mnamo Septemba 22, 2023.
Papa Francis akiwa Kanisa kuu la Notre-Dame de la Garde mnamo Septemba 22, 2023. © Daniel Cole / AP

Baada ya mazungumzo yake mafupi na mkuu wa serikali katika uwanja wa ndege, Papa Francis mara moja alielekea kwenye kanisa kuu la Notre-Dame de la Garde, kwenye miinuko ya mji wa Phocaea.

“Hatuwezi tena kushuhudia majanga ya ajali ya meli yanayosababishwa na biashara haramu ya kupindukia na ushabiki wa kutojali. Watu ambao wako katika hatari ya kuzama wakati wa kutelekezwa kwenye mawimbi lazima waokolewe. Ni wajibu wa binadamu, ni wajibu wa ustaarabu,” amesema kiongozi wa kanisa Katoliki duniani.

Siku ya Jumamosi, Papa atatoa hotuba ya mwisho ya Mikutano ya tatu ya Mediterania, baada ya matoleo ya Bari mnamo mwaka 2020 na Florence mnamo 2022.

Atakuna na rais Macron. Kabla ya kuondoka kwenda Roma, atatembea kwenye gari la papa kando ya Avenue du Prado, na aongoze misa katika uwanja wa Vélodrome.

Ziara hii ya Kiongozi wa kanisa Katoliki inafanyika chini ya ulinzi wa hali ya juu, karibu maafisa 6,000 wa polisi wamehamasishwa kama sehemu ya "mfumo wa ajabu", kulingana na afisa mkuu wa polisi.

Nchini Ufaransa, ziara ya Papa Francis imepokelewa kwa maono tofauti, linaeleza shirika la habari la AFP. Baadhi kutoka upande wa kulia wanakosoa "kuingilia" kwake kisiasa katika suala la uhamiaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.