Pata taarifa kuu

Papa Massata Diack, mwokozi au mchimba kaburi wa riadha duniani?

Kesi ya rufaa inayomkabili Papa Massata Diack, mtoto wa mkuu wa zamani wa Shirikisho la Riadha la Kimataifa, IAAF, Lamine Diack, anayeshukiwa kwa ufisadi na ubadhirifu, inakamilika Alhamisi mjini Paris kwa maombi ya mawakili wake ambao watamonyesha kama mwokozi wa shirika hilo la kimataifa.

Papa Massata Diack, mtoto wa mkuu wa zamani wa IAAF Lamine Diack akiwasili katika kituo kikuu cha polisi huko Dakar, Senegal, Jumatatu Februari 17, 2016.
Papa Massata Diack, mtoto wa mkuu wa zamani wa IAAF Lamine Diack akiwasili katika kituo kikuu cha polisi huko Dakar, Senegal, Jumatatu Februari 17, 2016. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mshauri huyo wa zamani wa Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF) mwenye umri wa miaka 57 alipatikana na hatia mwezi Septemba 2020 kwa kuhusika katika mpango wa hongo ili kuficha kesi za matumizi ya dawa za kusisimua misuli miongoni mwa wanariadha wa Urusi mwaka 2011. Alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na faini ya euro milioni moja. Anadai kutokuwa na hatia kutoka Senegal, ambapo anasema hawezi kuondoka kwa sababu yuko chini ya udhibiti wa mahakama katika kesi hii.

Siku ya Jumatano mwanasheria wa shirikisho la kimataifa, wakili Régis Bergonzi, alishutumu "ufisadi mkubwa" katika shirika lililoongozwa na Lamine Diack kati ya mwaka 1999 na 2015. Kulingana wakili huyo, rais wa zamani wa IAAF aliajiri mtoto wake wa kiume, na hivyo kuunda, yeye na washirika wake, mtandao wa ubadhirifu na ufisadi ili kuchelewesha taratibu za vikwazo dhidi ya wanariadha wa Urusi wanaoshukiwa kutumia dawa za kusisimua misuli, na hivyo kuwezesha baadhi yao kushiriki mashindano ya Olimpiki ya London mwaka 2012.

Kwa upande wake, wafadhili wa Urusi walisasisha mikataba yao ya ushirikiano na IAAF kwa mashindano ya kimataifa ya 2013 huko Moscow. Mikataba na benki ya Urusi VTB iliyosainiwa hadi 2015 ilifikia euro milioni 65.5. Lakini IAAF "ilipokea tu sehemu ya tano ya pesa zilizolipwa, au karibu euro milioni 13", amesema wakili Bergonzi. 

'Kesi kwa kesi'

Lakini kwa wanasheria wa Bw. Diack, tume hizi "zililingana" na umuhimu wa kandarasi, na ndiye aliyezishawishi taasisi kubwa kufadhili shirikisho lililokuwa na fedha duni wakati huo. "Tumeharibu heshima ya riadha na shirikisho", iliyopewa jina la World Athletics, amesema wakili Bergonzi, akiomba jumla ya euro milioni 41.2 kama fidia kwa uharibifu huo.

Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) iliomba euro ya mfano, shirika linalopambana na Dawa za Kuongeza Nguvu Duniani (WADA) kwa upande wake liliomba fidia ya euro 300,000 kwa washtakiwa sita, wanne kati yao wamehukumiwa katika Mahakama ya Rufaa na ni mmoja tu ambaye bado anasikilizwa.

Habib Cissé, mshauri wa zamani wa kibinafsi wa Lamine Diack, anakanusha kuwa alihusika katika suala la matumizi ya dawa za kuongeza nguvu kwa wanariadha wa Urusi. Siku ya Jumatano mbele ya mahakama, alihakikisha kwamba arifa kuhusu wanariadha kadhaa kwa shirikisho la Urusi (ARAF) zilishughulikiwa "moja baada ya nyingine", kulingana na kiwango cha tuhuma za utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu, na kwamba wanariadha wote wanaoshukiwa walisimamishwa.

Bw. Cissé, pia alipatikana na hatia ya kupokea euro milioni 3.45, kwa kosa la kuwaondoa wanariadha wa Urusi kwenye orodha ya wanariadha wanaoshukiwa kutumia dawa za kuongeza nguvu.

Wachunguzi walipata orodha nyumbani kwake iliyokuwa na majina ya wanariadha kadhaa na kiasi cha pesa. Pia waligunduwa mazungumzo kwa njia ya SMS na Papa Massata Diack ambapo lilikuwa ni swali la "malipo". "Kwa kweli uhahidi wa kutosha upo" alikiri, akihakikisha hata hivyo kwamba "hajawahi kuomba pesa".

Wafungwa wengine wawili kwa mara ya kwanza, rais wa zamani wa ARAF Valentin Balakhnitchev na afisa mwingine wa zamani wa michezo wa Urusi, Alexei Melnikov, pia wanashtakiwa tena bila kuwepo. Lamine Diack na mkuu wa zamani wa kupambana na dawa za kusisimua misuli katika shirika la IAAF, Mfaransa Gabriel Dollé, walifariki dunia tangu kuhukumiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.