Pata taarifa kuu
URAINE-OBAMA-PUTIN-MKATABA

Ukraine: Obama amtaka Putin kuheshimu mkataba wa amani

Rais wa Marekani Barack Obama amesisitiza Jumatatu hii wakati wa mazungumzo na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin juu ya haja ya kuheshimu makubaliano ya amani mashariki ya Ukraine.

Barack Obama katika Ikulu ya White Haouse Februari 22, 2016.
Barack Obama katika Ikulu ya White Haouse Februari 22, 2016. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mazungumzo kwa njia ya simu, Obama amesisitiza hasa umuhimu wa kuheshimu mkataba wa kusitisha mapigano na kuruhusu Ujumbe wa waangalizi wa Jumuiya ya uchumi na Maendeleo ya Ulaya OSCEkuhusu kutokuwa na uhuru wa kutembea katika eneo la mgogoro, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na serikali ya Marekani.

Pia Rais Obama amesisitiza haja ya kupatikana kwa makubaliano "haraka" juu ya taratibu za kuandaa uchaguzi "huru na wa haki" mashariki mwa Ukraine.

Kiev na nchi za Magharibi wanaituhumu Urusi kwamba inawapa silaha waasi wa Ukraine katika eneo la Mashariki na kuwa imetuma askari katika eneo la mgogoro, ambapo umesababisha maafa makubwa katika bara la Ulaya tangu vita vya Balkan katika miaka ya 1990.

Moscow imekana madai hayo, lakini mchango wake katika mgogoro wa Ukraine ulipelekea kuchukuliwa vikwazo vya kiuchumi na kudorora kwa uhusiano wake na nchi za Magharibi tangu mwisho wa vita baridi.

Washington imebaini wazi kwamba vikwazo hivyo vinaweza kufutwakatika miezi ijayo kama Urusi itatekeleza kikamilifu mikataba ya mwezi Februari 2015 iliyotiiliwa saini na Urusi, Ukraine, Ufaransa na Ujerumani katika mji wa Minsk.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.