Pata taarifa kuu
UFARANSA-CANADA-Ugaidi-Ushirikiano-Diplomasia

Canada na Ufaransa zashirikiana dhidi ya ugaidi

Ndege za kijeshi za Canada ziliyotumwa Mashariki ya Kati zimeendesha mashambulizi ya kwanza dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam kaskazini mwa Iraq.

Moja ya ndege ya kijeshi ya Canada ziliyoendesha mashambulizi ya kwanza nchini Iraq dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam.
Moja ya ndege ya kijeshi ya Canada ziliyoendesha mashambulizi ya kwanza nchini Iraq dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam. REUTERS/Vincenzo Pinto/Files
Matangazo ya kibiashara

Ni mashambulizi ya kwanza ya jeshi la Canada tangu ijiunge katika muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani dhidi ya Dola la wapiganaji la kiislam. Mashambulizi yanatokea wakati rais wa Ufaransa François Hollande yuko ziarani nchini canada.

Baada ya kuuzuru mji wa Alberta magharibi mwa Canada, Hollande amewasili mjini Ottawa. Siku ya leo itagubikwa na masuala ya usalama, ambayo Paris na Ottawa vina mtazamo sawa.

Wakati ambapo ndege za kijeshi za Canada zilikua zikiendesha mashambulizi yake ya kwanza nchini Iraq, Stephen Harper na François Hollande walikua wakikutana kwa mazungumzo. “ Mazungumzo ya viongozi hao wawili yaligubikwa na suala la ugaidi”, Ikulu ya Paris imesema.

Rais Hollande ambaye ni kutoka chama cha Kisoshalisti na Waziri Mkuu wa Canada, Harper ambaye ni kutoka chama cha Conservative wamekua na mtazamo sawa, licha ya kuwa François Hollande, amekua akiungwa mkono na wanasiasa kutoka vyama mbalimbali nchini Ufaransa, lakini Stephen Harper, amekua akikosolewa na wapinzani wake kwa kutuma wanajeshi Mashariki ya Kati ili kuendesha vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Vyama vya upinzani, vilipiga kura dhidi ya Canada kuingia katika muungano wa kimataifa dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam, mwezi mmoja uliyopita. Mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea wiki mbili zilizopita nchini Canada yaliibua mvutano kati ya wanasiasa na serikali nchini humo.

Rais wa Ufaransa, François Hollandeakiwa pamoja na  Waziri mkuu wa Canada,  Stephen Harper, Novemba 2 mwaka 2014mjini Banff.
Rais wa Ufaransa, François Hollandeakiwa pamoja na Waziri mkuu wa Canada, Stephen Harper, Novemba 2 mwaka 2014mjini Banff. REUTERS/Mike Sturk

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.