Pata taarifa kuu
SERBIA-KOSOVO-MAREKANI-USHIRIKIANO-UCHUMI

Trump atangaza kufikiwa mkataba kati ya Serbia na Kosovo juu ya 'kurejesha uhusiano wa kiuchumi'

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kwamba Serbia na Kosovo wamefikia makubaliano juu ya "kurejesha uhusiano wao wa kiuchumi" baada ya siku mbili za mazungumzo katika Ikulu ya White House.

Rais wa Marekani Donald Trump katika Ofisi ya ndogo ya Ikulu ya White House akiwa pamoja na rais wa Serbia Aleksandar Vucic na Waziri Mkuu wa Kosovar Avdullah Hoti Septemba 4, 2020.
Rais wa Marekani Donald Trump katika Ofisi ya ndogo ya Ikulu ya White House akiwa pamoja na rais wa Serbia Aleksandar Vucic na Waziri Mkuu wa Kosovar Avdullah Hoti Septemba 4, 2020. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Serbia na Kosovo wamejikubalisha kurejesha uhusiano wao wa kiuchumi," Trump amesema kutoka Ofisi ya White House, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi kuhusu sababu za mpango huo.

"Uchumi unaweza kuleta watu pamoja," amesema."Kwa kweli makubaliano haya ni ya kihistoria," ameongeza, mbele ya rais wa Serbia Aleksandar Vucic na Waziri Mkuu wa Kosovar Avdullah Hoti, ambao walikuwa wamekaa pembeni yake Ijumaa wiki hii.

Bwana Vucic kwa upande wake amebaini kwamba Bwana Trump alifanya "kazi nzuri" na amemwalika kuzuru Serbia.

Belgrade inakataa kutambua uhuru uliotangazwa na Kosovo mwaka 2008 baada ya vita mwishoni mwa miaka ya 1990, ambayo iligharimu maisha ya watu 13,000. Na Serbia inaungwa mkono na washirika wake Urusi na China, wakati Marekani ni miongoni mwa nchi zilizotambua mara moja taifa jipya la Kosovo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.