Pata taarifa kuu
SERBIA-COSOVO-MAZUNGUMZO-USHIRIKIANO

Kosovo na Serbia zaanza tena mazungumzo yanayodiwa kuwa magumu

Serbia na Kosovo zinaanza tena mazungumzo yao huko Brussels Alhamisi wiki hii baada ya kusitishwa kwa miezi kadhaa na migogoro ya mara kwa mara, lakini njia kuelekea kufufua uhusiano wao bado ni ngumu.

Waziri Mkuu wa Kosovo Avdullah Hoti na Rais wa Serbia Aleksandar Vucic.
Waziri Mkuu wa Kosovo Avdullah Hoti na Rais wa Serbia Aleksandar Vucic. AFP
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya miongo miwili, tangu mwisho wa vita ambavyo viliivunja Yugoslavia ya zamani (1998-99), mzozo huu bado ni hatari kwa utulivu wa ukanda huo.

Belgrade haitambui uhuru uliotangazwa mnamo mwaka 2008 na mkoa wake wa zamani wa kusini, wenye wakazi wengi wa jamii kutoka Albania. Makubaliano mengi ya kurejesha uhusiano yaliyofikiwa mnamo mwaka 2013 hayajazaa matunda yoyote.

Kosovo yenye wakazi Milioni 2 inatambulika kama nchi huru na nchi nyingi za Magharibi, ikiwa ni pamoja na nchi 22 kati ya 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU), lakini Urusi na China haziitambui kama nchi huru, hali ambayo inaendelea kuzua mvutano kwenye Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wa Serbia, hali hiyo ni kikwazo katika mchakato wa kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Baada ya mazungumzo mwishoni mwa juma lililopita, Rais wa Serbia Aleksandar Vucic na Waziri Mkuu wa Kosovo Avdullah Hoti wanakutana ana kwa ana leo Alhamisi huko Brussels, nchini Ubelgiji.

Ni mkutano wa kwanza rasmi wa aina hii tangu msimu wa joto mwaka 2019 wakati mkutano wa kilele huko Berlin kati ya Aleksandar Vucic na mwenzake wa Kosovo Hashim Thaçi haukuzaa matunda yoyote. Hashim Thaç, kigogo katika siasa za Kosovo tangu uhuru wa nchi hiyo, hajashirikishwa katika mazungumzo yoyote kutokana na mashtaka ya uhalifu wa kivita dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.