Pata taarifa kuu
AFRIKA-G20-CORONA-UCHUMI

G20 yasitisha kwa muda malipo ya madeni kwa mataifa masikini

Mei 1, 2020, riba zote kuhusu madeni ambayo yanapaswa kulipwa na mataifa 77 masikini, yakisaidiwa na Benki ya Dunia, zitabaki kwenye hazina zao. Na hiyo ni kwa muda wa miezi sita ... lakini muda wa miezi sita unaweza kuongezwa. Hatua hiyo ilimechukuliwa ili kila nchi ikabiliane na athari za janga la Covid-19.

G20 wamekubaliana kushirikiana kwa karibu na kutumia sera zilizopo kupunguza athari za janga la virusi vya corona na kuimarisha juhudi za kuupiga jeki uchumi wa dunia.
G20 wamekubaliana kushirikiana kwa karibu na kutumia sera zilizopo kupunguza athari za janga la virusi vya corona na kuimarisha juhudi za kuupiga jeki uchumi wa dunia. AFP/Jekesai Njikizana
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa fedha wa kundi la mataifa yaliyostawi kiuchumi na kiviwanda, G20, wamekubaliana kushirikiana kwa karibu na kutumia sera zilizopo kupunguza athari za janga la virusi vya corona na kuimarisha juhudi za kuupiga jeki uchumi wa dunia.

Kulingana na Bruno Le Maire, Waziri wa Fedha wa Ufaransa, dola bilioni 14 zitahifadhiwa kwa muda na nchi 77 masikini, baada ya uamuzi uliofanywa na mawaziri na mabenki kuu kutoka nchi za G20 Jumatano, Aprili 15.

Kiwango hicho ni riba ya madeni kwa nchi hizo, ambazo hazitalazimika kulipa kwa muda wa miezi sita (pamoja na miezi sita inayoweza kuongezwa baadaye).

Hatua hiyo itasaiodia kuepusha mdororo wa kiuchumi unaochochewa na janga la virusi vya Corona pamoja na kuongezeka kwa miito ya nafuu ya madeni kwa mataifa masikini yakiwemo ya Afrika.

Mkutano huo umefanyika siku moja baada ya mataifa saba yenye nguvu kubwa kiuchumi, G7, kusema yataunga mkono kusitishwa kwa muda malipo ya madeni kwa mataifa hayo masikini.

Ufaransa yakaribisha maamuzi "ya kihistoria"

Paris imebaini kuwa hii ni hatua ya kwanza ambayo inaweza kupelekea kufutwa kwa madeni nchi kwa nchi.

Wakati huo huo Ufaransa imesema iko tayari kuyasaidia mataifa ya Afrika kukabiliana na janga la maambukizi ya Corona.

Katika mahojiano maalum na RFI Kifaransa, rais Emmanuel Macron amesema anatambua kuwa mataifa ya Afrika yanakabiliwa na hali ngumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.