Pata taarifa kuu
TANZANIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Tanzania yathibitisha visa vipya 29 vya maambukizi

Serikali ya Tanzania imetangaza kwamba watu 29 wamepatikana na virusi vya Corona katika mji muu wa nchi hiyo, Dar es Salaam. Kufikia sasa Tanzania ina wagonjwa 88 walioambukizwa virusi vya Corona.

Mji wa Dar es-Salaam ambapo kumepatikana wagonjwa wapya 26 kati ya 29 waliothbitishwa nchini kote Tanzania..
Mji wa Dar es-Salaam ambapo kumepatikana wagonjwa wapya 26 kati ya 29 waliothbitishwa nchini kote Tanzania.. Wikimédia/Muhammad Mahdi Karim
Matangazo ya kibiashara

Wagonjwa 26 ni kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, wawili mjini Mwanza na mmoja katika eneo la Kilimanjaro kulingana na taarifa ya msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania.

Waziri ya Afya wa Tanzania Ummi Mwalimu amebaini kwamba wanawatafuta watu waliokaribiana na wagonjwa hao, huku akiongeza kwamba kufikia leo Jumatano takriban watu 11 wamepona virusi vya Corona, ambavyo mpaka sasa vimeua watu wanne.

Wakati huo huo Serikali imewataka raia wake kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Covid-19, na kuheshimu kanuni za usafi.

Kufikia sasa nchi ya Kenya inaongoza kwa wagonjwa wa Covid-19 katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo ina wagonjwa zaidi ya 215.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.