Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-UCHUMI

Ramaphosa atangaza mfululizo wa hatua za "kufufua" uchumi

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza mfululizo wa hatua za kufufua uchumi wa nchi yake ambao unaendelea kudorora, ikiwa ni pamoja na kulegeza hatua za kutoa visa ili kuongeza idadi kubwa ya watalii nchini humo na kuangalia upya mpango wa miundombinu.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mkutano wa BRICS huko Johannesburg Julai 27, 2018.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mkutano wa BRICS huko Johannesburg Julai 27, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mpango wa "miundo mbinu na kufufua Uchumi", uliotangazwa leo Ijumaa, una lengo la "kurejesha imani ya wawekezaji, kuepuka kufutwa kwa nafasi kadhaa na kutoa ajira mpya," Rais Ramaphosa amesema.

Afrika Kusini ambayo ni nchi inayostawi kiuchumi barani Afrika ina watu waliopoteza ajira ambao wamefikia sasa zaidi ya 27%.

Mpango huu hauendani na ongezeko la matumizi au gharama ya umma lakini "marekebisho ya vipaumbele vya bajeti ya sasa" ambayo yanahusiana na "karibu Rand bilioni 50" (sawa na Dola bilioni 3.5, au Euro bilioni 2.9), Rais Ramaphosa amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.