Cyril Ramaphosa: Hakuna ukoloni mamboleo katika misaada ya China
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amefutilia mbali kile anachoeleza "ukoloni mamboleo" kuhusu msaada wa China kwa Afrika. China imekua ikishtumiwa wakati mwingine kuongeza madeni kwa bara la Afrika.
Imechapishwa:
Katika kongamano la saba la kiuchumi kati ya China na Afrika Jumatattu wiki hii," Rais Ramaphosa almetetea uwepo wa China katika bara al Afrika, wakati Rais Xi Jinping akitangaza kutoa dola bilioni 60 kwa maendeleo ya Afrika.
Mkutano, ambao viongozi zaidi ya hamsini kutoka Afrika wanakutana na rais wa China, "unafutilia mbali hoja kwamba ukoloni mamboleo umewekwa barani Afrika, kama wanavyopenda kusema wapinzani," amesema Bw Ramaphosa.
President @CyrilRamaphosa addresses the Opening Ceremony of the FOCAC Beijing Summit 2018 #FOCAC2018 #BetterAfricaBetterWorld pic.twitter.com/qMRZ4DBfKD
PresidencyZA (@PresidencyZA) September 3, 2018
Lakini neno "ukoloni mamboleo" lilizungumzwa hivi karibuni kuhusu mikopo mikubwa inayotolewa na Beijing kwa nchi zinazoendelea kwa miradi ya miundombinu. Mikopo hii inaweza kuwa na ugumu kwa kulipa, na hivyo kuongeza hatari kwa mkopo kwa nchi zinazonufaika.