Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA-SIASA

Serikali ya Ethiopia yatetea uamuzi wa kutangaza hali ya hatari

Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia ametetea uamuzi wa Serikali kutangaza hali ya hatari nchi nzima wakati huu viongozi wa upinzani wakiandaa maandamano makubwa kupinga hatua hii ya Serikali.

Maandamano ya raia wa Etiopia kutoka jamii ya Oromos dhidi ya serikali, Oktoba 1, 2017 huko Bishoftu.
Maandamano ya raia wa Etiopia kutoka jamii ya Oromos dhidi ya serikali, Oktoba 1, 2017 huko Bishoftu. ZACHARIAS ABUBEKER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri Workneh Gebeyehu amewaambia wanadiplomasia wa kimataifa kuwa Serikali ililazimika kuchukua hatua hiyo ili kuleta utulivu na kuzuia jaribio lolote la kutatiza uchumi wa taifa hilo.

Akizungumza na shirika la habari la Marekani VOA, Waziri wa Mawasiliano wa Ethiopia Negeri Lencho, amesema chama tawala kinapambana na viongozi wala rushwa na kwamba hivi karibuni wananchi watarajie mabadiliko makubwa ikiwemo kufikishwa mahakamani kwa maofisa wa umma.

Mwishoni mwa juma lililopita waziri mkuu Hailemariam Desalegn alitangaza kujiuzulu nafasi yake kwa kile alichosema ni kupisha mabadiliko na kuleta maridhiano nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.