Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA

Waziri Mkuu wa Ethiopia ajiuzulu

Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ametangaza kujiuzulu baada ya kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa chama chake cha Ethiopia People's.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn. Photo: Reuters/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa haijafahamika kwamba chama chake kimekubali uamuzi huo au la.

“Nimechukua uamuzi wa kujiuzulu ili kusaidia kusuluhisha mzozo wa kisiasa uliopo nchini”, amesema Bw Desalegn.

Kujiuzulu kwa Desalegn kunakuja wakati ambapo kumeshuhudiwa maandamano ya miezi kadhaa dhidi ya serikali katika maeneo makuu nchini humo Oromia na Amhara.

Katika ghasia za mwisho zilizoshuhudiwa, watu 10 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika maandamano ya upinzani.Mamia ya watu walisadikiwa kuuawa katika machafuko hayo, huku wengine wakizuiliwa.

Ethiopia imeshuhudia maandamano mengi yaliokumbwa na ghasia tangu mnamo 2015, huku waandamanaji wakiitisha mageuzi ya kisiasa na kiuchumi na kutaka rushwa isitishwe serikalini.

Serikali imekua ikinyooshewa kidole cha lawama kwa kukandamiza upinzania na kuminya uhuru wa kujieleza nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.