Pata taarifa kuu
DRC-UCHUMI-UFISADI

Paradise Papers: Viongozi wa DRC wanyooshewa kidole kukwepa kodi

Uchunguzi mpya wa waandishi wa habari wa Taaisi moja inayofwatilia ukwepaji kodi unaofanywa na matajiri duniani inayofahamika kama "Paradise Papers" imefichua visa vya ukwepaji kodi nchini DRC ambapo viongozi mbalimbali wanahusishwa kwa mstari wa mbele.

makao makuu ya serikali ya DRC Kinshasa.
makao makuu ya serikali ya DRC Kinshasa. JUNIOR KANNAH/AFP
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi huo umeonyesha kuwa kampuni moja ya kimataifa kutoka Uswisi Glencore inayojihusisha na biashara ya madini kwenye migodi ya Shaba nchini DRC imekuwa ikiendeleza ufujaji mkubwa wa mali za nchi hiyo.

Kampuni hiyo inamilikiwa na mfanyabiashara wa Israeli ambaye amekuwa akishirikiana na wakuu wa serikali katika kukwepa kulipa kodi.

Tuhuma hizi zionatolewa siku chache baada ya shirika la kimataifa la Global Witness kuelezea kuwa madini mengi yamekuwa yakitolewa katika jimbo la Katanga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.