Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-SIASA

Hali ya sintofahamu yaendelea kuikumba DRC

Shughuli za kawaida zimeanza kurejea polpole asubuhi mjinu Bukavu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya mgomo wa siku nzima siku ya Jumatano.

Ofisi za manispaa ya jiji la Bukavu jiji la Bukavu, RDC.
Ofisi za manispaa ya jiji la Bukavu jiji la Bukavu, RDC. Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Benki, shule, vituo vya mafuta na maduka vilifungwa kwa lengo la kuendeleza shinikizo za kumtaka rais Jospeh Kabila kuondoka madarakani kufikia mwisho wa mwaka huu.

Mapema wiki hii hali kama hiyo ilishuhudiwa mjini Goma.

Reubens Mikindo, Naibu Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha UDPS amesema wananchi wameamua kuchukua hatua mikononi mwao.

Hayo yakijiri hofu imeendelea kutanda kwa mashirika ya misaada katika jimbo la Tanganyika mashariki nchini Jamuhiri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo asilimia 20 ya wananchi wamekimbia makwao, kwa mujibu wa shirika linaloshughulikia wakimbizi kutoka Norway.

Viongozi wa shirika hilo wanasema licha ya kupungua kwa mapigano hali bado ni mbaya na itaendelea kuwa mbaya zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.