Pata taarifa kuu

Kiwango cha ushiriki katika uchaguzi wa urais nchini Ufaransa chafikia 69.42%

Raia wa Ufaransa wanapiga kura kumchagua rais mpya kati ya wagombea 11. Miongoni mwa wagombea hao watatu ndio wanapewa nafasi kubwa ya kushiriki duru ya pili ya uchaguzi, kama hatapatikana mshindi katika uchaguzi huu. Watatu hao ni Emmanuel Macron, Marine le Pen na Jean-Luc Melenchon.

Wapiga kura Milioni 47 wanaamua ni nani atakayemrithi rais Francois Hollande ambaye mwaka uliopita, alitangaza kutotetea nafasi yake.
Wapiga kura Milioni 47 wanaamua ni nani atakayemrithi rais Francois Hollande ambaye mwaka uliopita, alitangaza kutotetea nafasi yake. Emmanuelle NICOLAS
Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura Milioni 47 wanaamua ni nani atakayemrithi rais Francois Hollande ambaye mwaka uliopita, alitangaza kutotetea nafasi yake.

Wagombea hawa watatu wakuu hawana historia yoyote ya kisiasa. Mpinzani wao mhafidhina Francois Fillon, amehudumia serikali katika nyadhfa kadhaa za uwaziri katika kipindi cha miongo miwili.

Usalama umeimarishwa kote nchini humo kuhakikisha kuwa zoezi hili linafanyika na kumalizika salama.

Mpaka sasa kiwango cha ushiriki kimefikia 69.42%

Wadadidi hao wanaeleza kuwa ushindani mkali zaidi utakuwa kati ya mgombea binafsi Emmanuel Macron, na mgombea wa chama cha Front National Bi. Marine Le Pen.

Huu ni uchaguzi unaoangaziwa kwa karibu sana kote duniani, hasa baada ya baada ya mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini Marekani baada ya Donald Trump kuibuka mshindi lakini pia Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Hata hivyo, wachambuzi nchini humo wanasema kuwa Marine Le Pen na Emmanuel Macron huenda wakamaliza katika nafasi ya kwanza na ya pili na kumenyana katika mzunguko wa pili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.