Pata taarifa kuu
UCHAGUZI UFARANSA 2017

Ufaransa: Wagombea 11 wachuana kwenye mdahalo wa mwisho wa TV tukio la kigaidi latia doa

Wagombea 11 kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kuingia ikulu ya Ufaransa wamewasilisha mikakati yao wakati wa mdahalo wao wa mwisho wa televisheni kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wenyewe Jumapili hii.

Wagombea 11 wa nafasi ya urais nchini Ufaransa ambao wamechuana kwenye mdahalo wa mwisho wa Televisheni. 20 April, 2017
Wagombea 11 wa nafasi ya urais nchini Ufaransa ambao wamechuana kwenye mdahalo wa mwisho wa Televisheni. 20 April, 2017 路透社
Matangazo ya kibiashara

Wagombe kutoka mrengo wa kulia Marine Le Pen na mwenzake mwenye misimamo mikali Jean-Luc Melenchon waliweka wazi ukosoaji wao kuhusu jumuiya ya umoja wa Ulaya na kwamba ikiwa watachaguliwa suala hili litakuwa kwenye ajenda zao za awali kabisa.

Hata hivyo mdahalo huu baadae ulifunikwa na tukio la kigaidi lililotekelezwa jijini Paris ambapo mshambuliaji mmoja na polisi waliuawa.

Mgombea mwenye msimamo wa kati Emmanuel Macron na mwenzake mwenye wa mrengo wa kushoto François Fillon kwa pamoja walitoa heshima zao na pole kwa askari aliyeuawa wakati wa makabiliano ya jijini Paris.

Macron amesema “jukumu la kwanza la rais ni kuwalinda raia” huku Fillon akisema ataahirisha kampeni zake za Ijumaa hii ambayo ndio siku ya mwisho ya kampeni.

Mgombe Marine Le Pen pia ametangaza kuahirisha kampeni zake za mwisho kutokana na tukio hili.

Kura za maoni zinaonesha kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa mgumu na wenye ushindani, huku karibu asilimia 30 ya wapiga kura wakiwa hawajaamua mpaka sasa watamchagua nani.

Wadadisi wa mambo wanasema uchaguzi wa mwaka huu wa Ufaransa ni moja kati ya chaguzi ambazo hazitabiriki kwa kiwango kikubwa na kwamba mdahalo huu ulikuwa ni nafasi ya mwisho kwa wagombea hawa kuongea na taifa.

Marine Le Pen na Emmanuel Macron ndio wagombea wanaoonekana kupewa sana nafasi ya kushinda kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi na kwamba huenda wakachuana wao wawili kwenye duru ya pili mwezi May.

Hata hivyo wagombe wengine Francois Fillon na mwenzake Jean-Luc Melechon nao wameongeza umaarufu wao hivi karibuni na kuwafuatia kwa karibu Le Pen na Macron.

Mdahalo wa safari hii ulikuwa tofauti na midahalo mingine, ambapo kila mgombea alihojiwa binafsi kwa dakika 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.