Pata taarifa kuu
HAITI-SIASA

Jovenel Moise aibuka msindi katika uchaguzi wa Urais nchini Haiti

Jovenel Moise ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Haiti katika duru ya kwanza, kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa Jumanne hii Novemba 29 na Baraza la Muda la Uchaguzi (CEP). Rais mpya ametoa wito kwa Wahaiti kuungana kwa ujenzi wa nchi yao.

Jovenel Moise, wakati wa hotuba yake ukifuatiwa na kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais wa Haiti.
Jovenel Moise, wakati wa hotuba yake ukifuatiwa na kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais wa Haiti. HECTOR RETAMAL / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ninatoa wito kwa vijana wa nchi hii, kwa Wahaiti wote wanaoishi nje ya nchi, kwa wataalamu wote nchini, kushirikiana bega kwa bega na mimi ili kuleta maendelea katika nyanja mbalimbali za nchi hii, kwa sababu Haiti inakabiliwa na matatizo mengi," amesema rais mpya wa Haiti, Jovenel Moise, kutoka hoteli ya kifahari katika mji wa Port-au-Prince, mji mkuu wa Haiti, dakika chache baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.

Mgombea aliyechaguliwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Michel Martelly ili kukiwakilisha chama chake cha PHTK ameshinda uchaguzi wa urais wa tarehe 20 Novemba 2016 katika duru ya kwanza, akipata 55.67% ya kura, kwa mujibu wa tangazo lililotolewa Jumatatu na wajumbe wa Baraza la Muda la Uchaguzi (CEP).

55.67% ya kura katika duru ya kwanza

Jude Celestin wa chama cha Lapeh, amechukua nafasi ya pili, akipata 19,52% ya kura, wakati ambapo Moise-Jean Charles akipata 11.04% ya kura na Maryse Narcisse, mgombea wa chama cha Fanmi Lavalas alipata 8.99%, kulingana na uder Antoine, afisa mkuu wa Baraza la Muda la uchaguzi (CEP).

Kuchaguliwa kwa Jovenel Moise, mwenye umri wa miaka 48 ambaye ni mwekezaji katika sekta ya kilimo imekua sasa ni mwanzo wa kazi yake ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.