Pata taarifa kuu
HAITI-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Haiti: Martelly katika duru ya pili Jumapili

Nchini Haiti, duru ya pili ya uchaguzi wa rais na wabunge itafanyika Jumapili Januari 24. Rais anayemaliza muda wake Michel Martelly na Waziri wake Mkuu Paul Evans wamefutiliwa mbali Alhamisi hii kuahirishwa tena kwa uchaguzi, licha ya kuongezeka kwa maandamano yenye vurugu na kukataa kwa upinzani kushiriki katika uchaguzi.

"Tuko tayari kwa uchaguzi Jumapili hii," amesema Rais Michel Martelly, Alhamisi, Januari 21, 2016.
"Tuko tayari kwa uchaguzi Jumapili hii," amesema Rais Michel Martelly, Alhamisi, Januari 21, 2016. AFP PHOTO/HECTOR RETAMAL
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la Rais Martelly katika makala kwenye redio na runinga ya taifa:

"Tuko tayari kwa ajili ya uchaguzi Jumapili hii. Kuhusu Jude Célestin, kwa kawaida, suala la kushiriki kwake linapaswa kuulizwa Jude Célestin mwenyewe. Sisi, kwa upande wa serikali, tuna wajibu wa kuandaa uchaguzi. Lakini kwa bahati mbaya, wakati inaonekana kuwa kuna mtu ambaye si kutoka upinzani anaweza kushinda, hali inabadilika na upinzani unanzisha wazo la kuwa kuna udanganyifu au wizi wa kura uliofanyika katika duru ya kwanza.

Tunaweza kutaja tabia hiyo kuwa ni njama kubwa yenye lengo la kutudhoofisha na hali hii inadumu kwa zaidi ya miaka miwili. Upinzani unatafuta kutupotezea muda ili tujikute kumeingia katika hali yenye utata Februari 7, hali ambayo haijaelezwa na Katiba. Watu wa upinzani wanataka kuweka mbele maslahi yao, ili wachukuwe madaraka kwa njia zao, kwa sababu hawawezi kuchukua madaraka kupitia uchaguzi", Rais wa Haiti Michel Martelly amesema.

Mchezo wa kuigiza

Hotuba ya Rais Martelly ilitangazwa kuwa itatolewa Jumatano usiku wiki hii; raia wengi wa Haiti walikuwa wanatarajia kuwa rais atatangaza kuahirishwa tena kwa uchaguzi.

Katika siku za hivi karibuni, hali sintofahamu imekua ikitanda nchini Haiti. Kwa sasa inaonekana mgombea atakua mmoja pekee katika uchaguzi wa urais: Jovenel Moïse. Mwengine, Jude Célestin, amekataa kushiriki katika uchaguzi huo, kwa madai ya udanganyifu mkubwa katika duru ya kwanza. Kujiuzulu kwa wajumbe wa Tume ya muda ya uchaguzi. Kugomea kwa mashirika ya waangalizi wa uchaguzi. Na hatimaye, azimio la Baraza la Seneti dhidi yauchaguzi wa Jumapili ijayo.

Uchaguzi au machafuko, kwa mujibu wa Paul Evans

Kutokana na ukosolewaji mkubwa dhidi ya serikali, Rais Michel Martelly amejibu. Rais huyo anaona kuwa ni "njama" ya upinzani, ambao hauwezi "kuchukua madaraka kupitia uchaguzi" na unataka "kutupotezea muda."

Nae Waziri Mkuu Paul Evans amesema kuna njia mbili tu zinazowezekana: kwenda kwenye uchaguzi Januari 24, au machafuko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.