Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI

Zoezi la kujiandikisha kwa wapiga kura laendelea DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, maandalizi ya uchaguzi yanaendelea, hata kama tarehe ya uchaguzi haijulikani. Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) imetangaza kuongeza muda wa zoezi la kuorodhesha wapiga kura katika mikoa saba mipya. Operesheni hii ilianza Julai 30 katika mkoa wa Nord-Ubangui.

Maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakati wa uchaguzi wa uraiswa mwaka  2011.
Maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakati wa uchaguzi wa uraiswa mwaka 2011. AFP PHOTO / SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hii pia imepelekea kupimwa kwa vifaa vilivyoagizwa kwa minajili ya uchaguzi. Corneille Nangaa, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI), amesema kuridhika: 'hadi sasa tumevuka idadi ya wapiga kura 500 000 waliojiandikisha na zoezi linaendelea kama kawaida.'

Kwamujibu wa Corneille Nangaa, udhaifu tuliouona katika zoezi la awamu ya kwanza ya vifaa vya uchaguzi tumeukosoa. Tumeagiza vifaa vingine. Masanduku 7,500 ya vifaa vitakavyotumika katika uchaguzi huo, ambavyo vinatarajiwa kuwasili wiki hii, vitapelekea kuanzisha operesheni katika mikoa saba mipya.

"Kwa vifaa hivyo, amesema Corneille Nangaa, tutahudumia mikoa saba mipya: Haut-Katanga, Lualaba na Haut Lomani pamoja na sehemu ya mkoa wa zamani wa Equateur, ni kusema, mkoa wa Sud-Ubangi, Tshuapa, Mongala na Equateur. "

CENI imeahidi kutekeleza ahadi zake: 'Kama tunaweza kupata msaada muhimu wa vifaa, tunaweza kwa uhakika kuokoa muda na kufupisha baadhi mambo. Jambo ambalo ni la uhakika, Julai 31, tutakuwa na faili kamili, zenye kuaminika na kuwa na mamlaka katika maandalizi yote ya uchaguzi.'

Kwa sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ina mikoa 26 baada ya kuongeza mikoa mingine. Zoezi la kuandika wapiga kura litatekelezwa katika mikoa 18 iliyobaki kama vifaa vya uchaguzi vikua vimekabidhiwa Tume Huru ya Uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.