Pata taarifa kuu
CONGO-UCHAGUZI-SIASA

Congo - Brazzaville: upinzani wagawanyika, miezi minne baada ya uchaguzi

Agosti 15 ni Siku Kuu ys kitaifa nchini Congo. Serikali ina matumaini ya kuifanya siku hii ishara ya umoja wa kitaifa. Hata hivyo miezi minne tu baada ya uchaguzi wa urais, baadhi ya wanasiasa wa upinzani bado wanapiga kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kwa Denis Sassou-Nguesso.

Guy Brice Parfait Kolelas mpinzani wa Rais Denis Sassou-Nguesso na mgombea aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais, Brazzaville Machi 17, 2016.
Guy Brice Parfait Kolelas mpinzani wa Rais Denis Sassou-Nguesso na mgombea aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais, Brazzaville Machi 17, 2016. MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika upinzani, wito wa mjadala wa kitaifa uliendelea kutolewa katika wiki za hivi karibuni, hata kama si kila mtu anakubaliana juu ya mkakati unaopaswa kutumiwa.

Miongoni mwa wanasiasa wa upinzani, kuna wale ambao bado wameendelea na msimamo wao wa kupinga uchaguzi wa Denis Sasou-Nguesso, ukianzia kwa Mathias Dzon. Miezi minne baada ya uchaguzi, Bw Dzon bado anakataa kumkubali Rais Sassou-Nguesso, na anaomba kuandaliwe uchaguzi mpya. Na huo ndio msimamo wa Claudine Munari. Kwa maoni yake, hakutakua na taasisi yoyote ya uongozi wa nchi kuanzia leo Jumatatu, kwani muhula wa Denis Sassou-Nguesso unamaizika Jumatatu hii Agosti 15. Mgombea huyo wa zamani sasa ni mkuu wa FROCAD.

Muungano mkuu wa vyama vya upinzani ulipoteza mshikamano wakati wa kampeni za uchaguzi. Mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani, Tstaty Pascal Mabiala, amekubali na "kuutambua" uchaguzi wa Rais Sassou tangu mwezi Aprili wakati, huku akiomba kama wengine mazungumzo chini ya mwamvuli wa jumuiya ya kimataifa. "Hakuna haja yoyote ya kuendelea kuangalia yaliyopita" amewajibu wale wanaomshtumu kunyenyekea haraka kwa kutafuta hadhi ya baadaye ya kuwa kiongozi wa upinzani. Jambo ambalo amekanusha.

Guy Brice Parfait Kolelas, aliyechukua nafasi ya pili katika uchaguzi wa uraisameendelea kusem akuwa uchaguzi wa urais uligubigwa na wizi wa kura. Itafahamika kwamba André Okombi Salissa, pia mgombea wa uchaguzi wa urais wa mwezi Machi, kwa mujibu wa wasaidizi wake, "amelazimishwa kukukimbilia mafichoni" kwa hofu ya "kukamatwa."

Ijumaa iliyopita, René Serge Blanchard Oba aliteuliwa kiongozi wa muda wa muungano wa vyama vya upinzani IDC kutokana na kukosekana kwa André Okombi Salissa. Kwa upande wa Jean-Marie Michel Mokoko, bado anazuiliwa jela. Mahakama itajadili Jumanne ombi la kuachiliwa kwake kwa dhamana lililotolewa na wanasheria wake. Bado anashtumiwa kosa la "kuhatarisha usalama wa taifa" na "kumiliki silaha za vita".

Denis Sassou Nguesso, Rais wa Congo Brazzaville akipiga kura mjini Brazzaville katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, Jumapili Machi 20, 2016.
Denis Sassou Nguesso, Rais wa Congo Brazzaville akipiga kura mjini Brazzaville katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, Jumapili Machi 20, 2016. © MARCO LONGARI / AFP

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.