Pata taarifa kuu
CONGO-MOKOKO

Jenerali Mokoko atuhumiwa kuhatarisha usalama

Nchini Congo - Brazzaville, mwanasiasa wa upinzani na aliyekuwa mgombea urais katika uchaguzi uliyopita, Jean-Marie Michel Mokoko, amewekwa jela.

Jenerali Jean-Marie Michel Mokoko.
Jenerali Jean-Marie Michel Mokoko. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Anashitakiwa kwa kuhatarisha usalama wa ndani wa nchi na kumiliki silaha na vifaa vingine vya kijeshi kinyume cha sheria. General Mokoko anashutumiwa kutaka kupanga mapinduzi mwaka 2007.

Jenerali Mokoko aliwekwa chini ya ulinzi Jumanne Juni 14 kwenye makao makuu ya polisi (DGST). Wiki iliyopita, Serikali iliomba utaratibu wa kimahakama uharakishwe.

Mkuu wa zamani wa majeshi ya Congo, mgombea aliyeshindwa katika uchaugzi wa urais, amehusishwa katika video iliyorekodiwa mwaka 2007 ikimuonyesha akijadili mpango wa kumtimua mamlakani Denis Sassou-Nguesso.

Siku tano zimekamilika Alhamisi hii baada ya kauli ya Waziri wa Sheria wa Congo, Pierre Mabiala, kumuomba Mwendesha mashitaka mkuu kuharakisha kesi dhidi ya jenerali Jean-Marie Michel Mokoko ili kesi hiyo imalizike. Mwanasiasa huyo a upinzani amewekwa chini ya ulinzi mapema Jumanne jioni kwenye makao makuu ya polisi (DGST), kwa mujibu wa mwanasheria wake Eric Yvan Ibouanga, ambaye hakutaka kutoa maelezo zaidi juu ya suala hili, ambalo bado liko kwenye hatua ya uchunguzi wa awali.

Jenerali Mokoko, Mkuu wa zamani wa majeshi ya Congo kati ya mwaka 1987 na 1993, mgombea aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais wa Machi 20, amehusisha katika video iliyorekodiwa mwaka 2007. Katika picha anaonekana akijadili mpango wa kumwondoa mamlakani Rais Denis Sassou-Nguesso.

Tangu uchaguzi wa rais, jenerali Mokoko alikua chini ya kifungo cha nyumbani nyumbani kwake katika jiji la Brazzaville. Ni katika makazi yake hayo ambapo polisi ilimkamata Jumanne jioni na kumpeleka moja kwa moja kwenye makao makuu ya polisi (DGST).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.