Pata taarifa kuu
UTURUKI-URUSI

Erdogan ziarani Urusi kufufua uhusiano na Putin

RAis wa Uturuki anazuru Urusi wakati ambapo, ameendekea kukosolewa kimataifa kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea kushuhudiwa nchini mwake.Hii ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu kushindwa kwa jaribio la mapinduzi Julai 15.

Vladimir Putin na Recep Tayyip Erdogan walipokutana mjini Ankara tarehe 1 Desemba 2014.
Vladimir Putin na Recep Tayyip Erdogan walipokutana mjini Ankara tarehe 1 Desemba 2014. REUTERS/Mikhail Klimentyev/RIA Novosti/Kremlin
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan atakutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin Jumanne Agosti 9.

Tangu Novemba, mahusiano kati ya mataifa hayo mawili yalikuwa yamedorora: Kitendo cha Uturuki kuangusha ndege ya kivita ya Urusi kilisababisha mvutano kati ya Ankara na Moscow. Kufufuliwa kwa uhusiano kati ya Urusi na Uturuki kumeukatisha tamaa Umoja wa Ulaya na Marekani.

Wiki chache zilizopita, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alimuandikia barua mwenzake wa Urusi. Rais wa Uturuki alimtaka mwenzake wa Urusi kusamehe yaliyopita na kufufua ukurasa mpya wa kidiplomasia wenye nguvu zaidi. Hatua ya pili ya leo Jumanne: wakuu hao wa nchi watakutana katika mji wa St Petersburg.

Erdogan ziarani nchini Urusi wakati ambapo mazingira ya ndani yamekua yakikosolewa katika nchi yake. Kwa upande wa Urusi, ziara hii inaonyesha umuhimu wa kimkakati kwa Uturuki. Masuali ambayo yanaweza kujadiliwa ni mengii: Suala la Syria kwanza, ambalo linaendelea kuzigawa nchi hizo mbili, fidia iwezekanayo baada ya uharibifu wa ndege ya Urusi na bila shaka kuanzishwa kwa mahusiano ya kiuchumi.

Viongozi hao wawili pia watajadili ushirikiano wa kinishati. "Urusi ni chanzo muhimu cha uagizaji wa nishati, amesema Ilya Lazarev, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya mchumi alipokua akihojiwa na RFI.

Baada ya jaribio la mapinduzi, Rais Erdogan aliona kuwa ametengwa na Umoja wa Ulaya na Marekani. Hata hivyo alisifu msimamo wa Vladimir Putin ambaye alimuunga mkono katika harakati zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.