Pata taarifa kuu
URUSI-UTURUKI

Urusi yatangaza mchakato wa kuweka sawa mahusiano na Uturuki

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wamesema Jumatano hii asubuhi Juni 29, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili mwezi Novemba.

Vladimir Putin.
Vladimir Putin. REUTERS/Alexander Zemlianichenko/Pool
Matangazo ya kibiashara

Ankara imebaini kwamba mazungumzo ya viongozi hao wawili "yalikua mazuri", na mkutano kati ya wawili hao umepangwa kufanyika hivi karibuni. Kremlin imethibitisha taarifa hii na imetangaza mchakato wa kuweka sawa mahusiano na Ankara.

Vladimir Putin, kwanza ametuma rambirambi zake kwa Rais Erdogan kuhusu shambulizi la mjini Istanbul. Kwa mujibu wa shirika la habari la INTRFAX, Kremlin inachunguza uwezekano wa mkutano kati ya marais hao katika siku za usoni.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa Uturuki, Erdogan na Putin wanapaswa kukutana mapema mwezi Septemba wakati wa mkutano nchi 20 ziliyoendelea kiuchumi (G20) nchini China. Na Moscow inakwenda mbali zaidi, ikisema kwamba kwamba vikwazo vya usafiri kwa Uturuki kwa raia wa Urusi vitaondolewa.

Vladimir Putin anasema amepokea dhamana zote muhimu za usalama kwa ajili ya watalii wa Urusi, licha ya vitisho vya ugaidi.

Moscow inaamua kusahau tukio la Novemba 24

Rais wa Urusi pia atatoa maelekezo kwa serikali kuanzisha mazungumzo ili kurejesha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili katika uchumi na biashara hasa. Kremlin inazungumzia mchakato wa kuweka sawa mahusiano na Uturuki.

Tayari, mkutano kati ya mawaziri wawili wa kigeni umepangwa kufanyika Ijumaa Julai 1 katika mkutano wa jumuiya ya Ushirikiano wa nchi zinazochangia Bahari Nyeusi utakaofanyika Sochi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.