Pata taarifa kuu
AUSTRIA-SIASA

Alexander Van der Bellen achaguliwa kuwa rais

Mgombea binafsi Alexander Van der Bellen, anayeungwa mkono na wanamazingira, ameshinda uchaguzi wa rais nchini Austria kwa 50.3% ya kura. Amemshinda mgombea kutoka mrengo wa kulia Norbert Hofer, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Austria amethibitisha Jumatatu hii Mei 23.

Mwanamazingira Alexander Van der Bellen amekua rasmi rais mpya wa Astria.
Mwanamazingira Alexander Van der Bellen amekua rasmi rais mpya wa Astria. REUTERS/Heinz-Peter Bader
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, Austria hatimaye imempata rais wake mpya. Rais huyo ni Alexander Van der Bellen, ambaye amejikusanyia 50.3% ya kura. Amemshinda kura 30 000 mpinzani wake Norbert Hofer wa chama cha FPO (Freedom Party) kutoka mrengo wa kulia. Chama hiki kimekubali kushindwa, kwenye akaunti yake ya Facebook.

Wizara ya Mambo ya Ndani ilisubiri kura zote zihesabiwe ili iweze kutangaza matokeo rasmi, Jumatatu, Mei 23 muda mfupi kabla ya 17h.

Mgombea kutoka mrengo wa kulia amesemai "kusikitishwa sana", ameelezea mwandishi wetu Nathanael Vittrant. Norbert Hofer ameweza kukusanya katika jina lake nusu ya wapiga kura wa nchi hiyo. alama ambazo vyama vingi vya kizalendo Ulaya vimekua vikifikiria.

Katika duru ya kwanza Aprili 24, Norbert Hofer alishinda kwa 35% ya kura dhidi ya 21% alizopata Alexander Van der Bellen. Wagombea wa vyama vya SPO na OVP, vyama hivi viwili vilivyotawala siasa ya Austria tangu mwisho wa Vita Kuu vya pili vya dunia, viliondolewa. Kabla ya zoezi la kuhesabu kura katika duru ya pili, Hofer alikua amepata 51.9% ya kura na Alexander Van der Bellen 48.1%.

Kwa Austria ni matokeo yasiyokuwa ya kawaida. Kamwe wanamazingira walikua hawajapata uongozi wa nchi. Lakini Alexander Van der Bellen ana mengi ya kufanya kwa kuiweka sawa nchi ya Austria iliyogawanyika.

Pongezi zaanza kumiminika

Tayari, rais anayemaliza muda wake, kutoka chama cha SPO, Heinz Fischer, amempongeza mshindi na kutangaza kuwa "amemualika" kumtembelea Jumanne katika Ikulu ya Hofburg, na "kuandaa zoezi la kukabidhiana madaraka", zoezi liliopangwa kufanyika Julai 8.

Nchini Ufaransa, Rais François Hollande amekaribishwa "kwa moyo mkunjufu" ushindi wa Alexander Van der Bellen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.