Pata taarifa kuu
Raga

Wachezaji wa raga nchini Kenya wasitisha mgomo

Wachezaji wa mchezo wa raga wa timu ya taifa ya Kenya yenye wachezaji saba kila upande, wamekubali kusitisha mgomo uliokuwa unaendelea kudai marupurupu yao.

Wachezaji wa Kenya wakisherehekea ushindi katika michuano iliyopita
Wachezaji wa Kenya wakisherehekea ushindi katika michuano iliyopita worldrugby/photo
Matangazo ya kibiashara

Kikosi hicho kimekuwa kikilamikia kutolipwa marupurupu yao ya msimu wa mwaka 2015-2016.

Serikali imekubali kulipa kiasi kikubwa cha deni la wachezaji hao ambao wanajiandaa kwa michuano ya Kimataifa.

Mgomo huu ulikuwa umetishia ushiriki wa Kenya kwenye michuano ya dunia ya HSBC inayoanza mwishoni mwa wiki hii huko Dubai na baadaye mjini Cape Town nchini Afrika Kusini.

Naibu Mwenyekiti wa chama cha mchezo huo Thomas Opiyo amethibitisha kutatuliwa kwa mgogoro huu.

Wachezaji hao walitaka kulipwa marupuru yao yanayokadiriwa kuwa Dola za Marekani 200,000 sawa na Shilingi Milioni 20 za Kenya.

Baada ya mzozo huo kutatuliwa, kocha mpya Innocent Simiyu amekitaja kikosi chake kinachosafiri baadaye Jumatatu kwenda Dubai.

Hata hivyo, mfugaji bora Collins Injera na Oscar Ouma wameachwa katika kikosi hicho.

Kikosi kamili:-
Dan Sikuta, Brian Tanga, Martin Owila, Andrew Amonde, Darwin Mukidza, Frank Wanyama, William Ambaka, Leonard Mugaisi, Cyprian Kuto, Augustine Lugonzo, Billy Odhiambo, Nelson Oyoo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.