Pata taarifa kuu
Raga

Uganda ndio bingwa wa Afrika mchezo wa raga kwa wachezaji 7 kila upande

Uganda ndio mabingwa wa mwaka huu wa taji la Afrika katika mchezo wa raga kwa wachezaji saba kila upande.

Timu ya taifa ya mchezo wa raga ya Uganda ikisherehekea baada ya kuibuka mabingwa barani Afrika Septemba 24 2016 jijini Nairobi nchini Kenya
Timu ya taifa ya mchezo wa raga ya Uganda ikisherehekea baada ya kuibuka mabingwa barani Afrika Septemba 24 2016 jijini Nairobi nchini Kenya ragahouse.com
Matangazo ya kibiashara

Cranes walinyakua taji hilo baada ya kuifunga Namibia kwa alama 38-19 mwishoni mwa wiki iliyopita, jijini Nairobi nchini Kenya.

Kocha Tobert Onyango amekisifu kikosi chake kwa mafanikio hayo makubwa ambayo wamekuwa wakiyatamani kwa muda mrefu.

Matokeo kamili yalivyokuwa :-
Fainali: Uganda 38-19 Namibia
Nusu Fainali: Kenya 12-17 Uganda

Ushindi huu wa Uganda unaipa nafasi ya kipekee  kufuzu katika michuano ya dunia ya World Sevens Series mwaka ujao huko Hong Kong.

Mbali na kufuzu katika michuano hiyo, Uganda pia itacheza katika fainali za Dubai Sevens mapema mwezi Desemba mwaka huu na wamejumuishwa pamoja na Afrika Kusini, Marekani na Scotland.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.