Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016-RAGA

Timu ya taifa ya mchezo wa raga ya Kenya yashindwa kuwika Brazil

Timu ya taifa ya mchezo wa raga ya Kenya yenye wachezaji saba kila upande, imepoteza michezo yake miwili katika hatua ya makundi kutafuta medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki inayoendelea nchini Brazil.

Timu ya taifa ya mchezo wa raga ya Kenya ikiwa uwanjani kumenyana na New Zealand
Timu ya taifa ya mchezo wa raga ya Kenya ikiwa uwanjani kumenyana na New Zealand Daily Nation
Matangazo ya kibiashara

Katika mechi ya kwanza, Kenya walifungwa na Uingereza kwa alama 31 kwa 7, huku wakipoteza mechi ya pili kwa alama 28 kwa 5 dhidi ya New Zealand.

Ni wazi kuwa kwa matokeo haya, itakuwa vigumu sana kwa timu ya Kenya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali.

Kenya ambayo ni ya mwisho katika kundi lake la C, inasubiri mechi yake ya mwisho dhidi ya Japan baadaye hivi leo.

Wawakilishi wengine wa Afrika, Afrika Kusini, wao wameshinda mechi zao zote na bila shaka kuelekea kufuzu katika hatua ya robo fainali baada ya kuishinda Uhispania kwa alama 24 kwa 0 na baadaye Ufaransa kwa alama 26 kwa 0.

Fiji inaongoza kundi la A kwa alama 6, baada ya kushinda mechi zake mbili za kwanza dhidi ya Brazil kwa alama 40 kwa 12 na Argentina kwa alama 21 kwa 14.

Ratiba ya mechi za leo kumaliza hatua ya makundi:-

Kundi A
Argentina vs Brazil
Fiji vs Marekani
Kundi B
Ufaransa vs Uhispania
Afrika Kusini vs Australia
Kundi C
Kenya vs Japan
New Zealand vs Uingereza

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.