Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016-RAGA

Fiji yashinda ubingwa wa mchezo wa raga

Timu ya taifa ya mchezo wa raga ya Fiji, yenye wachezaji saba kila upande ndio mabingwa wa Michezo ya Olimpiki kwa upande wa wanaume.

Kikosi cha timu ya taifa ya Fiji baada ya kushinda medali ya ghahabu katika michezo ya Olimpiki
Kikosi cha timu ya taifa ya Fiji baada ya kushinda medali ya ghahabu katika michezo ya Olimpiki OlympicOrg
Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha Fiji, kilijipatia medali ya dhahabu baada ya kuishinda Uingereza katika mchezo wa fainali Jumatano usiku kwa alama 43 kwa 7.

Fiji imeshinda taji hili kwa mara ya kwanza katika michezo hii ambayo pia imechezwa kwa mara ya kwanza katika historia ya michezo hii.

Mashindano ya kutafuta ubingwa yalichezwa kwa siku sita katika uwanja wa Deodoro jijini Rio de Janeiro.

Sherehe zimekuwa zikiendelea katika jiji kuu la Fiji, Suva katika nchi ambayo ina zaidi ya watu 900,000.

Fiji ikisherekea ushindi baada ya kushinda medali ya dhahabu
Fiji ikisherekea ushindi baada ya kushinda medali ya dhahabu olympic.org

Uingereza hata hivyo haijaondoka mikono mitupu katika michezo hii baada ya kujipatia medali ya fedha.

Wawakilishi wa Afrika, Afrika Kusini, wamemaliza katika nafasi ya tatu na kujishindia medali ya shaba baada ya kuishinda Japan kwa alama 54 kwa 14 kutafuta mshindi wa tatu.

Kenya ambayo pia iliiwakilisha bara la Afrika, iliondolewa katika hatua ya makundi baada ya kushindwa katika mechi zake zote.

Mataifa mengine yaliyoshiriki kwa upande wa wanaume ni pamoja na Brazil, New Zealand, Argentina, Marekani, Ufaransa, Australia na Uhispania.

Kwa upande wa wanaume, timu ya taifa ya Australia ilishinda medali ya dhahabu, New Zealand ikashinda ile ya fedha na Canada ya shaba.

Kenya ndio nchi pekee kutoka barani Afrika iliyowakilisha bara la Afrika katika michezo hii lakini ikaondolewa katika hatua ya makundi baada ya kufungwa na New Zealand, Uhispania na Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.