Pata taarifa kuu

Ligi ya Mabingwa: PSG yaibwaga Barcelona na kutinga nusu fainali dhidi ya Dortmund

Wakiongozwa kwa bao moja  toka dakika ya 12 kwenye kambi ya Nou, Paris SG wamewamenya FC Barcelona kwa mabao 4-1 baada ya kufukuzwa kwa beki wa kati wa klabu hiyo Ronald Araujo kufuatia madhambi aliyomfanyia Barcola baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Kylian Mbappé.

Kikosi cha wachezaji cha Paris Saint-Germain baada ya kuibwaga Barcelona.
Kikosi cha wachezaji cha Paris Saint-Germain baada ya kuibwaga Barcelona. REUTERS - Juan Medina
Matangazo ya kibiashara

Wakiongozwa kwa bao moja toka dakika ya 12 kwenye kambi ya Nou, Paris SG wamewamenya FC Barcelona kwa mabao 4-1 baada ya kufukuzwa kwa beki wa kati wa klabu hiyo Ronald Araujo kufuatia madhambi aliyomfanyia Barcola baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Kylian Mbappé.

Paris-SG watacheza kwa mara ya nne nusu fainali ya kihistoria katika ligi ya Mabingwa baada ya mwaka 1995, 2020, na 2021, lakini wametoka mbali. Baada ya kufungwa (2-3) wakati wa mechi ya awali katika uwanja wa Parc des Princes, klabu hii ya Ufaransa ilikuwa tayari ikiongozwa kwenye uwanja wa Barcelona toka dakika ya 12. Kwa wakati huo wa mchezo, mashabiki wachache wa PSG walikuwa wametabiri kuwa wachezaji wao watalazimika kufunga chondechonde mabao hata mawili ili waweze kuwasukuma FC Barcelona kuingia katika muda wa nyongeza. Lakini matumaini madogo yaligeuka kwa mshangao mkubwa na hivyo  kupata nafasi nzuri baada ya kufukuzwa kwa beki wa kati wa Barcelona Ronald Araujo baada ya kufanya madhambi.

Katika nusu saa ya mchezo, wakati vijana wa Xavi walikuwa wakitawala mchezo, beki wa Barcelona kutoka Uruguay, alipewa kadi nyekundu na hivyo kufukuzwa  baada ya kumfanyia madhambi Barcoka akiwa kwenye nafasi nzuri ya kuona lango la Barcelona. Blaugrana (Barcelona) ambao walikuwa wakiongoza toka dakika ya 12 kwa bao moja la Raphinha, ambaye alifunga mabao mawili katika mechi ya awali, walilazimika kukabiliana dhidi ya Mbappé na wachezaji wenzake. Na wakati Ousmane Dembélé  akisawazisha baada ya kupkea pasi kutoka kwa Bradley Barcola, katika dakika ya 40, hali ilibadilika.

Baada ya mapunziko, PSG walikuja juu na kushika kasi ya kuishambulia Barcelona. bao lapili la PSG lilifungwa na par Ousmane Dembélé kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 61.

Hata hivyo Barcelona hawakuchoka waliendelea kuishambulia PSG na hivyo kuwatia wasiwasi mashambiki wa PSG. Hata hivyo PSG iliweza kuingiza bao la tatu kufuatia mkwaju wa Mbappé katika dakika ya 90, na hivyo Bacelona kusalimu amri.

PSG watamenyana na Borussia Dortmund katika nusu fainali ndani ya wiki mbili. Klabu hii ya Ujerumani ambayo ilifungwa katika mechi ya awali kwenye uwanja wa Atlético Madrid (1-2), pia iliwabwaga wapinzani wake kwa mabao 4-2 wakiwa nyumbani. PSG Dortmund walikuwa katika kundi moja katika msimu huu katika ligi ya Mabingwa. PSG waliiwafunga Dortmundkatika mechi ya awali (2-0) kabla ya kupata pointi moja wakati wa mchezo wa marudio. Matokeo ambayo yanawapa matumaini ya kushinda mashabiki wa PSG.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.