Pata taarifa kuu
Ufaransa-SOKA

Euro 2016: Deschamps atangaza kikosi chake cha wachezaji 23

Mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la mataifa ya Ulaya (Euro 2016) Juni 10, kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, ametangaza Alhamisi hii usiku kikosi chake cha wachezaji 23.

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Ufaransa, Didier Deschamps,Novemba 12, 2015.
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Ufaransa, Didier Deschamps,Novemba 12, 2015. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Bw Deschamps hakuwataarifu wachezaji waliochaguliwa kuvaa jezi ya Blu ya timu ya taifa ya Ufaransa, amewashitukiza tu kwa kutangaza majina yao.

Wachezaji hao 23 ni akina nani ?

Makipa: Benoît Costil (Rennes), Hugo Lloris (Tottenham / ENG), Steve Mandanda (Marseille).

Mabeki: Patrice Evra (Juventus Turin / ITA), Christophe Jallet (Lyon), Laurent Koscielny (Arsenal / ENG), Bacary Sagna (Manchester City / ENG), Eliaquim Mangala (Manchester City / ENG), Jeremy Mathieu (Barcelona / ESP) Raphael Varane (Real Madrid / ESP), Lucas Digne (AS Roma / ITA).

Viungo wa Kati: Yohan Cabaye (Crystal Palace / ENG), Lassana Diarra (Marseille), Ngolo Kante (Leicester / ENG), Blaise Matuidi (Paris SG), Paul Pogba (Juventus Turin / ITA), Moussa Sissoko (Newcastle / ENG).

Washambuliaji: Kingsley Coman (Bayern Munich / GER), Andre-Pierre Gignac (Tigres Monterrey / MEX), Olivier Giroud (Arsenal / ENG), Antoine Griezmann (Atletico Madrid / ESP), Anthony Martial (Manchester United / ENG), Dimitri Payet (West Ham / ENG)

Wachezaji wa akiba: Alphonse areola (Villarreal / ESP), Hatem Ben Arfa (Nice), Kevin Gameiro (FC Sevilla / ESP), Alexandre Lacazette (Lyon), Adrien Rabiot (Paris SG), Morgan Schneiderlin (Manchester United), Djibril Sidibé ( Lille), Samuel Umtiti (Lyon)

Wachezaji ambao hawakushirikishwa

Mathieu Valbuena, ambaye hakuchaguliwa huichezea Ufaransa katika michuano ya Kombe la mataifa ya Ulaya mwaka huu (Euro 2016), alikuwa na "kiwango cha chini ya kile ambacho angeliweza kufanya" akiichezea klabu ya OL (Olympique Lyonnais), alisema kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps.

Msimu wa Mathieu Valbuena uliangushwa na jaribio la usaliti wa udhalilishaji ambao ulimponza. "Mathieu alikua na msimu mgumu zaidi katika klabu ya Olympique Lyonnais, alipata majeruhi mengi na kiwango chake utendaji kilikua chini ya kile ambacho angeliweza kufanya," amesema Deschamps, pia akizungumzia "ushindani wa wachezaji ambao ni mzuri zaidi "katika nafasi yake," ikiwa ni katika kikosi cha wachezaji 11 au wachezaji wa akiba. "

Vile vile Karim Benzema, mshambuliaji nyota wa Real Madrid, ambaye anafanyiwa uchunguzi kufuatia usaliti wa kingono dhidi ya Mathieu Valbuena na beki Mamadou Sakho kwa kosa la ukiukwaji wa kanuni zinazopiga marufuku dawa za kusisimua mwili, hawakushirikishwa katika timu ya taifa ya Ufaransa "Le Bleus".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.