Pata taarifa kuu
UFARANSA-SOKA-UEFA

Karim Benzema afanyiwa uchunguzi, pigo kubwa kwa “Les Blues”

Karim Benzema amefanyiwa uchunguzi Alhamisi hii kwa jaribio la kumshurutisha mchezaji mwenza wa timu ya taifa ya Ufaransa Mathieu Valbuena, kulipa pesa kwa watu fulani ili kuzuia ukanda wa ngono usichapishwe. Ni pigo kubwa kwa timu ya taifa ya soka ya Ufaransa ikiwa imesalia miezi saba ya Kombe la mataifa ya Ulaya.

Karim Benzema (katikati, akivalia kofia), akiondoka katika Ofisi ya mashtaka ya Versailles, karibu na mji wa Paris, Novemba 5, 2015.
Karim Benzema (katikati, akivalia kofia), akiondoka katika Ofisi ya mashtaka ya Versailles, karibu na mji wa Paris, Novemba 5, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Miaka mitano baada ya kesi inayojulikana kwa jina la "Zahia", iliyotamatika kwa kuachiliwa huru moja kwa moja mwaka 2014, kashfa hii mpya haimrahisishii kocha wa timu ya taifa ya soka ya Ufaransa, Didier Deschamps.

Wachezaji wote wawili pia hawakuitwa kwa mechi ya kirafiki ya tarehe 13 na 17 Novemba, dhidi ya Ujerumani na Uingereza. Valbuena hakushirikiswa katika mechi hizi kwa sababu "haiko katika hali nzuri kisaikolojia" wakati ambapo Benzema anuguza "jeraha", ameeleza Deschamps, ambaye amesema atakitaja kikosi chake cha wachezaji muda mfupi baada ya uamuzi wa jaji anayeendesha uchunguzi.

Benzema anachunguzwa kwa "jaribio la utapeli na makosa ya kushiriki katika kundi la wahalifu kwa ajili ya maandalizi ya kosa linaloadhibiwa kifungo cha miaka mitano jela, kosa ambalo ni utapelii ", Ofisi ya mashtaka ya Versailles imebaini. Mchezaji wa Real Madrid amewekwa chini ya uangalizi wa mahakama ikiwa ni pamoja na kukatwaza "kuwasiliana katika njia yoyote ile na mtu aliyetendewa kosa hilo pamoja na wengine ambao wanafanyiwa uchunguzi ".

Ofisi ya mwendesha mashtaka ya imekariri kuwa Benzema anachunguzwa kwa kosa la kushiriki njama ya kumtoza mchezaji mwenza pesa mbali na kujaribu kumshurutisha awalipe wasaliti hao fedha.

Benzema ametokea mlango wa nyuma wa jengo la mahakama ya Versailles kabla ya saa 7:00, waandishi wa habari wa shirika la habari la Ufaransa la AFP wameshuhudia. "Benzema amesema hana hatia", mwanasheria wake Sylvain Cormier, amehakikisha.

Duru zimeielezea shirika la habari la AFP kuwa tayari mshambulizi huyo wa Real Madrid amekiri kuhusika.

Inaaminika kuwa mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 27 alimshawishi Valbuena kuhusiana na ukanda huo kwa niaba ya rafikiye wa tangu utotoni.

Magazeti nchini Ufaransa yanadai kuwa Benzema alitaja ukanda huo wa ngono walipokuwa katika mazoezi ya mechi ya kimataifa wakiwa Clairefontaine mapema mwezi Oktoba.

Mshambuaji huyo amehakikisha kuwa "alitaka kumsaidi rafiki yake," bila kufikiri kuwa alimueweka hatiani Valbuena, chanzo kilio karibu na kes hiyo kimesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.