Pata taarifa kuu
UFARANSA-SOKA

Utapeli: Benzema chini ya ulinzi, kueleza kuhusika kwake

Mchezaji mwaminifu au mshirika wa kundi la masaliti? Karim Benzema amewekwa chini ya ulinzi Jumatano wiki hii na wakaguzi, ambao wanajiuliza kuhusu kuhusika kwake katika madai ya utapeli "sextape" dhidi ya nyota mwingine wa timu ya taifa ya Ufaransa, Mathieu Valbuena.

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Karim Benzema, wakati wa mazoezi kabla ya mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Armenia Oktoba 8, 2015 katika uwanja wa Allianz Riviera, jijini Nice.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Karim Benzema, wakati wa mazoezi kabla ya mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Armenia Oktoba 8, 2015 katika uwanja wa Allianz Riviera, jijini Nice. MATTHIEU ALEXANDRE/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Akivalia kofia juu ya kichwa, mshambuliaji wa Real Madrid ameripoti kwa siri kwenye kituo cha polisi cha Versailles, muda mfupi kabla ya 03:00 asubuhi ( saa za Ufaransa), waandishi wa habari wa shirika la habari la Ufaransa la AFP wamebainisha.

Katika uchunguzi huo: video inamuonyesha Valbuena, akizungukwa na kundi la watu ambao pia walimjaribu kushirikiana nao katika utapeli.

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na uchunguzi, Benzema alizungumzia video hiyo akiwa pamoja na Valbuena Oktoba 5, katika mkutano wa timu ya taifa ya Ufaransa katika jijini Clairefontaine kabla ya mechi dhidi ya Armenia na Denmark.

Watu hao watatu wanaoshukiwa kuwa matapeli, ambao wakati huu wanazuiliwa jela , waliwasiliana wakati huo na nmtu wa karibu na ndugu wa Benzema ili kumtumia mshambuliaji wa Real Madrid katika katika kundi lao la matapeli.

Wachunguzi wameamua kumuweka Benzema chini ya ulinzi ili kuamua kama katika mazungumzo ya Clairefontaine pamoja na Valbuena yalikua yanahusu " ushauri wa kirafiki uliolenga kumtaka aachane na tabia hiyo au kumlazimisha kulipa ", kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na uchunguzi.

" Karim Benzema hajishuku chochote, kwani hahusiki katika kesi hiyo na "ni mwenye furaha, na ni mwenye kuridhika, kwa kuweza hatimaye kukomesha utata huu unaoonyesha sra mbaya ", Sylvain Cormier mwanasheria wake. " Yuko pale ili kujibu maswali ya wakaguzi ", Sylvain Cormier ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.