Pata taarifa kuu
UFARANSA-Michezo

Eric Abidal ajiondoa katika timu ya taifa ya Ufaransa

Baada ya Franck Ribéry, hatimaye beki wa timu ya taifa ya Ufaransa, Eric Abidal ametangaza kwamba amesitisha kuichezea timu hiyo, baada ya kutengwa katika michuano ya kombe la dunia 2014 iliyochezwa nchini Brazil.

Eric Abidal, beki wa timu ya taifa ya Ufaransa, achukua uamzi wa kutoichezea tena timu hiyo.
Eric Abidal, beki wa timu ya taifa ya Ufaransa, achukua uamzi wa kutoichezea tena timu hiyo. AFP
Matangazo ya kibiashara

“Nimechoshwa. Sijafanya mkutano na waandishi wa habari, na sijazungumza lolote kuhusu hatua yangu hii. Leo ni kwa mara yangu ya kwanza ninazungumzia hatua hii. Lakini siniko tayari kuichezea tena timu ya taifa ya Ufaransa”, Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona amesema jumatano jioni wiki hii kwenye redio ya Catalan Rac1.

Abidal ambaye alisumbuliwa na maradhi ya ini katika mwaka 2012, na ambaye hakushirikishwa katika michuano ya kombe la dunia 2014, amesema uamzi wake huo unafaa.

“Kocha wa timu ya taifa Didier Deschamps aliniita na kunieleza kwamba sinimo kwenye orodha ya kikosi cha taifa kitakacho shiriki michuano ya kombe la dunia, kauli hiyo ilinigusa kwa kweli”, ameongeza Abidal.

Eric Abidal, alianza kukata tamaa wakati klabu ya Barcelona aliyokua akichezea kukataa kuomuongezea muda wa mkataba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.